KLABU ya PAS Lamia ya
Ugiriki limemtaka mchezaji wa kimataifa wa Sierra Leone John Kamara
kutofanya mazoezi au kucheza katika klabu hiyo kwa muda wa wiki tatu kwa
hofu ya ugonjwa wa Ebola. Kamara alirejea nchini Ugiriki baada ya
kuitumikia nchi yake katika michezo miwili ya kufuzu michuano ya Mataifa
ya Afrika iliyofanyika nchini Cameroon. Klabu hiyo ilimuambia Kamara
kuwa uamuzi huo umekuja kufuatia ushauri wa wizara ya afya ya nchi
hiyo. Kamara amesema Lamia wamemwambia apumzike kwa siku 15 mpaka 21 ili
waweze kuona maendeleo yake baada ya kutoka Afrika kuitumikia nchi
yake. Sierra Leone walilazimika kuandaa mchezo wao wa nyumbani nchini
Cameroon katika jiji la Younde kwasababu ya nchi hiyo kufungiwa kucheza
nyumbani na Shirikisho la Soka la Afrika-CAF kutokana na mlipuko wa
ugonjwa wa Ebola. Kamara amesema wakati wako nchini Cameroon walikuwa
wakichekiwa joto la mwili kila asubuhi na jioni na aliwaweka wazi Lamia
kuwa wamfanyie vipimo vyovyote kwani anajua hajaambukizwa Ebola lakini
hawakutaka hivyo inabidi aheshimu uamuzi wao.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumamosi, 18 Oktoba 2014
Home
/
Unlabelled
/
EBOLA.....NYOTA WA SIERRA LEONE ASIMAMISHWA NA KLABU YAKE HUKO UGIRIKI BAADA YA KUTOKA KUTUMIKIA TIMU YAKE YA TAIFA.
EBOLA.....NYOTA WA SIERRA LEONE ASIMAMISHWA NA KLABU YAKE HUKO UGIRIKI BAADA YA KUTOKA KUTUMIKIA TIMU YAKE YA TAIFA.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni