STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 3 Oktoba 2014

KLABU YAMCHARUKIA MALINZI, ZAPANGA KUGOMEA JEZI ZA VODACOM, AZAM TV, ZATISHIA KUMVUA URAIS

DK NDUMBARO AKIWA MAKAO MAKUU YA FIFA.
Siku moja baada ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi kusisitiza lazima klabu zikatwe asilimia 5 kwenye fedha zao za udhamini wa Vodacom na Azam TV, zenyewe zimejibu mapigo.

Kupitia mwanasheria wao, klabu 14 za Ligi Kuu Bara, zimesisitiza mambo haya ya msingi, kuwa hazitavaa jezi zenye nembo ya wadhamini hao, kupinga kukatwa fedha zao.
Pili, zitaitisha mkutano wa dharura wa kamati ya utendaji kupiga kura ya kutokuwa na imani na Malinzi ambayo itamuondoa madarakani.
Mwanasheria maarufu nchini Dk Damas Daniel Ndumbaro amesema kwa mujibu wa katiba ya TFF, klabu hizo 14 ambazo ni mwanachama zinaruhusiwa kufanya hivyo.
“Hilo linaruhusiwa kwa mujibu wa ibara ya 25 (ibara ndogo ya TFF) kama wanachama tuitishe mkutano mkuu maalum.
“Katika mkutano huo tutapiga kura za kutokuwa na imani na Malinzi, kinachotakiwa ni kufikia theluthi mbili tu, yaani kura mia moja,” alisema Ndumbaro.
TFF ina wanachama 150, hivyo kama utaitishwa na kufikisha theluthi hizo mbili za kura ya kutokuwa na imani, Malinzi atakuwa ameng’oka madarakani.
Uamuzi wa klabu hizo kupinga umetokana na kwamba TFF kupitia sekretarieti yake iliyodai ni kwa mujibu wa kamati ya utendaji, imepitisha uamuzi wa kutaka ipewe asilimia 5 ya fedha za udhamini za klabu.
Jambo hilo halijafanyika sehemu yoyote duniani, pia kumekuwa hakuna ufafanuzi mzuri wa kutosha zaidi ya Malinzi kusisitiza kuwa ni lazima fedha hizo zikatwe.
Kiutaratibu inaonyesha klabu ndiyo zinazotangaza wadhamini hao, ndiyo zenye haki ya fedha hizo.
Lakini katika mapato ya milangoni, fedha zimekuwa zikikatwa fedha ambazo zinakwenda kwenye mfuko wa maendeleo ya soka nchini ambao sasa TFF unataka ukate na fedha za wadhamini.

Mbeya City na Mtibwa Sugar, zimetishia kuifikisha TFF mahakamani kama itaendelea kulazimisha uamuzi huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox