STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 3 Oktoba 2014

BAADA YA KUPIGA HAT-TRICK WELBECK SASA AANZA KUCHONGA.

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Danny Welbeck amewakosoa waajiri wake wa zamani Manchester United kwa kusisitiza kuwa walikwamisha kiwango chake kwa kumchezesha kama winga wakati akiwa huko. Mameneja wa United akiwemo Sir Alex Ferguson, David Moyes na Louis van Gaal wote walimtumia Welbeck kama mshambuliaji wa pembeni huku Van Gaal akifafanua hivi karibuni kuwa nyota huyo hakufunga mabao ya kutosha. Lakini Welbeck amekuwa katika kiwango cha juu toka alipohamia Arsenal kwa kitita cha paundi milioni 16 na sasa amefunga mabao manne katika mechi tano alizocheza baada ya kufunga mabao matatu au hat-trick katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray. Akihojiwa Welbeck amesema hakuna yoyote anayeweza kumkosa moja kwa moja kwasababu hawajawahi kumuona akicheza katika ya ushambuliaji wa kati mara kwa mara. Welbeck aliendelea kudai kuwa sasa anapata nafasi hiyo na anachofanya ni kutumbukiza mipira katika wavu kama ilivyo kwa washambuliaji wengine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox