STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 9 Oktoba 2014

UBAGUZI WA RANGI KATIKA SOKA UINGEREZA UKO WAZI - WEBB.

MKUU wa kikosi kazi cha kupambana na na ubaguzi wa rangi wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Jeffrey Webb amedai kuwa ubaguzi katika soka la Uingereza uko wazi. Webb ubaguzi huo unaonekana kwa kukosekana kwa watu wenye asili ya kiafrika katika nafasi muhimu katika soka la nchi hiyo. Mapema ofisa mkuu wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa, Gordon Taylor alifafanua kuwa ubaguzi ni suala lilijificha sana katika soka la nchi hiyo. Lakini kauli yake hiyo imepingwa vikali na Webb na kudai kuwa sio la lililojificha kwani liko wazi mbele ya macho yao na hakuna mtu anayetaka kulifanyia kazi. Webb ambaye pia ni kiongozi wa shirikisho la soka kwa nchi za Carribean na Amerika Kaskazini na Kati alimtolea mfano kocha wa timu ya vijana ya Chelsea Eddie Newton. Newton mwenye umri wa miaka 42, alikuwa akifanya kazi chini ya Roberto di Matteo wakati Chelsea walipotwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2012 lakini hakufanyiwa mahojiano yoyote. Webb amesema kwa kitendo kama hicho haoni kama ubaguzi ni suala lililojificha kama inavyodaiwa bali liko wazi na hatua makusudi zinapaswa kuchukuliwa ili kulitatua.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox