STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 9 Oktoba 2014

ROMA WAKALI KULIKO JUVENTUS - PALLOTTA.

RAIS wa AS Roma, James Pallotta anaamini klabu hiyo ni imara zaidi kuliko mabingwa watetezi wa Serie A Juventus. Kikosi cha Roma kinachonolewa na kocha Rudi Garcia kilitandikwa mabao 3-2 na mabingwa hao wa Italia jijini Turin Jumapili iliyopita lakini Pallotta anaamini kuwa utata na ugumu wa mchezo huo unaonyesha wazi kuwa timu hizo sasa zinalingana kiviwango. Akihojiwa Pallotta amesema kwa maono yake anadhani Roma wako imara zaidi ya Juventus na mchezo wa uliopita umeonyesha ushahidi kamili kwenye hilo pamoja na kwamba walipoteza. Rais huyo aliendelea kudai kuwa anajua Juventus ni timu imara lakini wana wachezaji wa kiwango kama hicho kama sio zaidi nab ado waliwakosa wachezaji wao muhimu kama Davide Astori, Kevin Strootman na Daniele De Rossi. Roma kwasasa wako katika nafasi ya pili katika msimamo wa Serie A wakiwa na alama 15 katika michezo sita waliyocheza, wakitamnguliwa na vinara Juventus kwa tofauti ya alama tatu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox