STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 16 Desemba 2014

Nani mtani jembe! Maximo, Msaidizi wake na Emerson watupiwa virago kama Brandts, Pluijm arejeshwa. Cortinho abaki Tambwe ndani

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYI0JOOV_DLYIBPKikljbikHszNzNjCbxoxz8iiVEnGgUSwXu6vsgtF5TzycxQJ061DpGQ0sxFrZ9wrdWHYJpRoMDyzDgndqXAuJgocAJZtO1iN6FUukesrB-S5qFrA_f8tpOyvu8znxaW/s1600/DSC_0306.JPG
Marcio Maximo na msaidizi wake Leonardo Neiva wakati wakiinoa Yanga

KAMA ilivyokuwa kwa kocha Ernie Brandts aliyetimuliwa baada ya Yanga kufungwa na Simba kwenye mchezo wa 'bonanza' wa Nani Mtani Jembe, hali hiyo imemkuta Marcio Maximo.
Kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars kutoka Brazil ametimuliwa Yanga baada ya kipigo cha mabao 2-0 katika pambano la Nani Mtani Jembe-2.
Taarifa ambazo ni za uhakika toka ndani ya Yanga zinasema kuwa, kocha Maximo amepewa mkono wa kwaheri na nafasi yake inarudi kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo  Hans Van Der Pluijm.
Mmoja wa viongozi wa kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga amesema, Maximo ataondoka nchini ndani ya siku tatu baada ya kukubaliana na uongozi.  
"Si kwamba amefukuzwa, lakini ni makubaliano kwamba anaondoka.  
"Ni kweli, lakini msitake kulikuza hili jambo ionekane kama tumemfukuza," aliuliza na alipotakiwa kujua mrithi ni nani, alikataa kusema.  
Hata hivyo ni kwamba Maximo amepewa mkono wa KWAHERI sambamba na kiungo aliyekuja naye toka kwao, Emerson Oliveira ambaye inaelezwa amekosa ITC japo ukweli ni kwamba ameonekana ni bomu.
Yanga ilimfurusha Brandt na wasaidizi wake, Fred Felix Minziro na Razack Ssiwa baada ya timu yao kulala mabao 3-1 na safari hii Maximo anaondoka na wasaidizi wake akiwamo Mbrazil mwenzake Leonardo Neiva ambaye alimleta baada ya kusaini mkataba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox