STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 5 Desemba 2014

UNITED YAMHAKIKISHIA VAN GAAL FUNGU LA USAJILI KAMA AKIHITAJI.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal amehakikishiwa kuwa pesa sio tatizo kama akiamua kuimarisha kikosi chake katika kipindi cha majira ya kiangazi. Van Gaal alitumia kitita cha paundi milioni 150 katika majira ya kiangazi, ukiwemo usajili uliovunja rekodi Uingereza wa paundi milioni 59.7 kwa ajili ya Angel Di Maria lakini bado wanaburuzwa na vinara Chelsea kwa tofauti ya alama 11 katika msimamo wa Ligi Kuu. Kiungo wa ulinzi Kevin Strootman na mabeki Mats Hummels na Diego Godin wote wako katika rada za United. Hata hivyo, Ofisa Mkuu wa United Ed Woodward tayari ameshweka wazi kuwa hatataka kuchukua mchezaji kwa mkopo katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo Januari. Woodward alibainisha mwezi uliopita kuwa tayari wana wachezaji waliowalenga kwa ajili ya usajili ujao wa majira ya kiangazi ila yoyote atakayeweza kupatikana Januari watafanya mipango ya kumchukua.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox