STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 4 Desemba 2014

WENGER AMMWAGIA MISIFA KEMKEM SANCHEZ BAADA YA KUOKOA JAHAZI JANA.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa hakuna mchezaji yeyote katika Ligi Kuu aliyezoea mazingira haraka kuliko Alexis Sanchez. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea Barcelona Julai amefunga bao lake la tisa kwa msimu huu jana wakati rsenal ikiibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Southampton. Wenger amesema ni vigumu kutafuta mfano wa mchezaji aliyezoea haraka mazingira kama ilivyo kwa Sanchez kwani amekuwa na uchu wa ushindi. Sanchez sasa anakuwa amefunga mabao 14 katika mechi 22 za mashindano yote alizoichezea Arsenal toka ajiunge nao akitokea Camp Nou kwa kitita cha paundi milioni 35. Akiwa Barcelona Sanchez aliifungia mabao 47 katika mechi 141 huku akiifungia nchi yake mabao mawili katika michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Brazil majira ya kiangazi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox