STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 8 Januari 2015

PSG INAWEZA KUMSAJILI MESSI - PASTORE.

MCHEZAJI nyota wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG, Javier Pastore amesema timu hiyo iko tayari kumsajili Lionel Messi kama mshambuliaji huyo wa Barcelona atawekwa sokoni na kudai kuwa pesa haitakuwa tatizo. Messi amekuwa na uhusiano wa kuyumbayumba na klabu hiyo msimu huu jambo ambalo limezua maswali kuhusiana na mustakabali wake huku tetesi hizo zikiongezeka baada ya kuondoka kwa wakurugenzi wa michezo Andoni Zubizarreta na Carles Puyol wiki hii. Messi mwenyewe alikaririwa mapema msimu huu akidai kuwa pengine anaweza kuondoka Barcelona katika siku za usoni na Pastore anaamini kuwa PSG itakuwa tayari kumsajili nyota huyo pindi nafasi itakapotokea. Pastore amesema kama itatokea Messi kuondoka Barcelona anadhani mmiliki wa PSG atakuwepo kujaribu kumsajili mchezaji huyo kwani pesa sio tatizo kutokana na rasilimali zilizopo katika klabu hiyo. Messi ana mkataba na Barcelona mbao unaishia katika majira ya kiangazi mwaka 2018 lakini kama itatokea kuondoka klabu itakayotaka kumsajili italazimika kutoa kitita cha euro milioni 250.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox