STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 5 Januari 2015

SIMBA YA ZAMALEK KUCHEZA KUMCHANGIA CHRISTOPHER ALEX

Wachezaji wa Simba ambao walishiriki katika kikosi kilichoing’oa Zamalek mwaka 2003 wameamua kumchangia mwenzao Christoper Alex Massawe.


Massawe yu mgonjwa taabani kwao Dodoma. Hali ambayo imewafanya Simba walioifunga Zamalek, Massawe akifunga penalti ya mwisho iliyoihakikishia Simba ushindi.

Kiungo huyo anaumwa na imeelezwa anasumbuliwa na kifua kikuu ingawa bado jambo hilo halijatolewa ufafanuzi na familia yake.

Boniface Pawasa ambaye alicheza namba tano katika mechi hiyo amesema wanaandaa mechi ya kirafiki.

“Lengo ni kupata mechi ambayo itamsaidia ndugu yetu kupata matibabu.

“Wikiendi hii tunaweza kucheza pale Karume kama hakutakuwa na mechi ya daraja la kwanza. Hili ni jukumu letu, wadau wajitokeze.


“Tayari baadhi ya waliocheza siku hiyo wamejitokeza, Emmanuel Gabriel na Victor Costa tumeishakubaliana," alisema.

Credit: Saleh Jembe

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox