STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 5 Januari 2015

TETESI ZA USAJILI ULAYA: MADRID KUMUACHIA VARANE KWA PAUNDI MILIONI 20, LIVERPOOL KUMREJESHA ORIGI, CITY YAMPIGIA HESABU DRAXLER.

KATIKA habari za tetesi za usajili zilizopamba vichwa vya habari katika mitandao na magazeti barani Ulaya, mojawapo ni klabu za Chelsea na Manchester United zimepashwa kuwa zitalazimika kulipa kitita cha paundi milioni 20 kama watahitaji sahihi ya beki wa Real Madrid Raphael Varane. Kwingineko klabu ya Liverpool inajipanga kuilipa kitita cha paundi milioni tatu klabu ya Lille kwa ajili ya kumrejesha mshambuliaji Divock Origi mwezi huu. Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 19 sasa yuko katika mkataba wa msimu mzima na klabu hiyo ya Ufaransa. Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini anataka kumsajili kiungo wa klabu ya Schalke Julian Draxler ingawa klabu hiyo ya ujerumani inataka kitita cha paundi milioni 25 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. Kiungo mkongwe wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard mwenye umri wa miaka 34 amepiga chini ofa yenye thamani ya paundi milioni 18 kwa ajili ya kwenda kucheza soka nchini Qatar wakati atakapoondoka Anfield mwishoni mwa msimu huu. Tukibakia hapohapo Anfield, Liverpool inatarajia kutenga kitita cha paundi milioni 23 kwa ajili ya mshambuliaji wa klabu ya West Bromwich Albion Saido Berahino mara watakapomuuza Fabio Borin. Kwa upande wa Tottenham Hostpurs wao wanaripotiwa kujiandaa kumuuza golikipa wao Hugo Lloris mwenye umri wa miaka 28 kwa kitita cha paundi milioni 25. Nchini Hispania kiungo mahiri wa Barcelona Sergio Busquets mwenye umri wa miaka 26 anajipanga kuzinyong’onyesha klabu za Arsenal, Chelsea na Manchester United zinzomuwinda, kwa kusaini mkataba mpya na kllabu hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox