STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 30 Juni 2015

LAPORTA AJINADI KUIREJESHA TENA NEMBO YA UNICEF KATIKA FULANA ZA BARCELONA.

RAIS wa zamani wa Barcelona, Joan Laporta amejinadi kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha analirejesha jina la UNICEF au shirika lolote la misaada ya kibinadamu katika fulana za timu hiyo kama akirejea tena madarakani katika uchaguzi wa mwezi ujao. 

Laporta ndiye aliyetengeneza dili la UNICEF miaka 10 iliyopita wakati akiwa rais kuanzia mwaka 2003 mpaka 2010 ambapo ilishuhudia nembo ya shirika hilo ikiwekwa katika fulana za timu hiyo kwa mara ya kwanza katika historia. 

Chini ya uongozi uliopita, ulioongozwa na Sandro Rosell na baadae Josep Maria Bartomeu umeshuhudia nembo ya wadhamini ya shirika la ndege la Qatar ikionekana mbele ya fulana huku nembo ya UNICEF ikiwekwa nyuma. 

Akijinadi katika kampeni za uchaguzi, Laporta amesema atafanya kila awealo kuhakikisha anatafuta wadhamini ambao wataweza kufanikisha hilo na kurejesha nembo ya UNICEF katika fulana za timu hiyo tena. 

Laporta anakabiliwa na upinnzani mkali kutoka kwa rais aliyepita Bartomeu katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Julai 18 mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox