STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 29 Juni 2015

SCHWEINSTEIGER AIZODOA MAN UNITED.

KIUNGO wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger amesema anataka kushinda taji la nne mfululizo ya Bundesliga akiwa na timu hiyo, pamoja na tetesi zinazomhusisha na kwenda klabu ya Manchester United. 

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 anamaliza mkataba wake kiangazi mwakani na alicheza katika mechi 20 za Bundesliga msimu uliopita na 28 katika mashindano yote wakati Bayern walipofanikiwa kunyakuwa taji la tatu la ligi mfululizo. 

Ingawa bado hajakubali kusaini mkataba mpya na Bayern, Schweinsteiger amesema anataka kushinda taji lingine la Bundesliga akiwa na Bayern msimu ujao. 

Kiungo huyo amekuwa akihusishwa na tetesi za kujiunga na United katika majira haya ya kiangazi hatua ambayo ingemuwezesha kuungana na kocha wake wa zamani Louis van Gaal ambaye amemfundisha wakati akiwa Bayern. 

Hata hivyo kauli yake ya kutaka kunyakuwa taji la nne la Bundesliga akiwa na Bayern inafifisha tetesi hizo za kwenda United kiangazi hiki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox