STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 20 Julai 2015

ALICHO KISEMA VAN GAAL KUHUSU CHICHARITO


Kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal amemtaka mshambuliaji wake raia wa Mexico, Javier Hernandez 'Chicharito' kufunga mkanda kama anahitaji kudumu kikosini hapo.

Hernandez ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika klabu ya Real Madrid, hivi sasa amerejea na anatarajiwa kujiunga kambini na wenzake 25 Julai huko nchini Marekani.

Van Gaal ambaye hakuona nafasi ya Hernandez kikosini hapo msimu uliopita mara baada ya uwepo wa washambuliaji Radamel Falcao Garcia, Robin Van Persie huku Wayne Rooney pia akicheza nafasi hiyo.

Van Gaal akiongea na waandishi wa habari wikiendi hii amethibitisha kumpa nafasi Hernandez, lakini akasisitiza anatakiwa atumie nafasi hiyo.

Hadi sasa United wana Rooney, Wilson na Hernandez pekee kama washambuliaji wa kati lakini Van Gaal yuko relaxed akiamini ni wakati wa Rooney sasa kuongoza jahazi.

Wakati huo huo klabu ya Manchester United iko mbioni kusaka saini ya golikipa Sergio Romero wa timu ya taifa ya Argentina aliyepo huru hivi sasa.


Sergio Romero ambaye amemaliza mkataba na klabu ya Sampdoria anawindwa pia na Real Madrid. United wanajiandaa kutafuta mbadala wa Victor Valdez ambaye anatimka klabuni hapo baada ya kukosana na kocha Louis Van Gaal.

Maoni 3 :

  1. Kwangu ni sawa kupewa nafasi kwa mara nyengine tena kijana wetu #GGMUNITED

    JibuFuta
  2. Kwangu ni sawa kupewa nafasi kwa mara nyengine tena kijana wetu #GGMUNITED

    JibuFuta
  3. Kwangu ni sawa kupewa nafasi kwa mara nyengine tena kijana wetu #GGMUNITED

    JibuFuta

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox