STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 24 Julai 2015

WAKALA ASEMA BENZEMA KUTUA ARSENAL NI JAMBO LA KUCHEKESHA


Hatimaye wakala wa mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema amethibitisha kuwa uwezekano wa nyota huyo kuihama klabu yake ya Real Madrid na kujiunga na Arsenal ni jambo la kuchekesha.

Wakala huyo amethibitisha kuwa ana zaidi ya 1000% kwamba Benzema atabakia klabuni hapo kwa muda mrefu zaidi.

Taarifa hizo zimekuja kama mkuki ndani ya moyo wa mashabiki wa Gunners ambao wiki hii yote walikua na matumaini ya kumpata nyota huyo.

Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Olympic Lyon ya Ufaransa, amekuwa katika headlines kwa muda sasa tangu kuwasili kwa kocha Rafa Benitez kikosini hapo, ambapo tetesi zimekuwa zikidai huwenda Cristiano Ronaldo akacheza nafasi ya Karim Benzema, ushambuliaji wa katikati.

Mshambuliaji huyo ambaye ni mfaransa amekuwa akihusishwa sana na kutua Emirates, lakini kauli hizi za agent wake zinazima ndoto za kocha Arsene Wenger pamoja na mashabiki kwa ujumla.

Klabu ya Arsenal imekuwa ikikosolewa mara kwa mara kutokana na kukosa mtu mwenye uwezo wa kufunga na kuwatesa mabeki wa timu pinzani na sasa wanahaha kutafuta mtu.


Aidha legendari wa klabu hiyo ya Arsenal, Thierry Henry amekua haridhishwi na uwezo wa mshambuliaji wa sasa wa gunners, Oliver Giroud.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox