STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 5 Agosti 2015

DANI ALVES AKABIDHIWA JEZI YA XAVI.

BEKI wa mahiri wa Barcelona, Dani Alves amekabidhiwa jezi namba sita iliyokuwa ikitumiwa na Xavi kufuatia kuondoka kwa kiungo huyo mkongwe katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi. 

Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil amekuwa akivaa jezi namba 22 kwa msimu kadhaa iliyopita kwa heshima ya mchezaji mwenzake wa zamani Eric Abidal, lakini sasa ameamua kuchukua namba ya nyota huyo wa zamani wa Hispania. 

Kwa upande mwingine Mbrazil mwenzake Douglas yeye amepewa jezi namba mbili kufuatia kuondoka kwa Martin Montoya kwenda Inter Milan mapema kiangazi hiki huku Munir na Sandro nao wakipewa jezi za kikosi cha kwanza ambazo ni namba 17 na 16. 

Golikipa Marc-Andre ter Stegan anatarajiwa kuendelea kuvaa jezi namba moja, wakati golikipa aliyekuwa chaguo la kwanza msimu uliopita yeye ataendelea na namba 13. 

Wachezaji wapya waliosajiliwa Arda Turan na Aleix Vidal wao hawatapewa namba kwasasa mpaka hapo watakapoanza kucheza Januari mwakani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox