STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 5 Agosti 2015

TERRY ANATAKA KUFUATA NYAYO ZA GIGGS.

BEKI wa Chelsea, John Terry amedai kuwa amekuwa akifanya mazoezi kwa bidii kwa miaka kadhaa ili kujiweka fiti kwani anataka kucheza soka kwa kipindi kirefu kama ilivyokuwa kwa kiungo wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs. 

Giggs aliamua kutundika daruga akiwa na umri wa miaka 40 baada ya kuitumikia United kwa kipindi cha miaka 23 na kupewa kibarua cha kocha msaidizi wa timu hiyo akiwa chini Louis van Gaal msimu uliopita. 

Terry mwenye umri wa miaka 34 amekuwa sehemu muhimu katika kikosi cha Chelsea kilichotwaa taji la Ligi Kuu msimu uliopita na bado ana mipango ya kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa kipindi kirefu kijacho. 

Akihojiwa Terry amesema katika kipindi cha miaka minne mitano iliyopita amekuwa akifanya kazi ya ziada sio katika mazoezi ya uwanjani pekee bali pia nje ya uwanja na kuhakikisha anakula chakula sahihi. 

Beki huyo aliendelea kudai kuwa anafanya hivyo kwakuwa anajua kuna nafasi ya kucheza kwa kipindi kirefu kama ilivyokuwa kwa Ryan Giggs.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox