Goli
pekee la Christian Benteke katika uwanja wa Anfield lilitakiwa
kukataliwa kwasababu mchezaji mwenzie, Philippe Coutinho alikuwa tayari
ameotea.
Siku
chache kabla ya msimu mpya kuanza, yalifanyika mabadiliko ya sheria ya
kuotea ambapo mchezaji yoyote anayecheza mpira katika eneo la kuotea,
kibendera lazima kiwe juu na hata kama hakugusa mpira.
Philippe Coutinho alikuwa ameotea wakati mpira wa krosi uliochongwa na Jordan Henderson unajaa ndani kutoka winga ya kushoto
Coutinho alijaribu kumalizia krosi hiyo kabla ya kumfikia Benteke, lakini hakuna kibendera kilichoonekana juu.
Mwamuzi msaidizi, Harry Lennard alishindwa kunyosha kibendera, akimuacha Benteke afunge.
Neville amedai makosa haya ni stori za kila msimu na kila msimu mpya wanakuja na mabadiliko lakini hakuna wanachofanya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni