Baada ya Juma Nyosso kumfanyia
vitendo vya udhalilishaji mchezaji wa Azam FC na timu ya Taifa John
Bocco ‘Adebayor’, mchezaji wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga Amir
Maftah amesema, hata yeye alishawahi kukumbana na kitendo kama hicho
kutoka kwa Nyosso na kusema mchezaji huyo amezoea kwani tayari
ameshafanya hivyo kwa wachezaji wengi.
“Unajua mpira unapochezwa
uwanjani dakika 90 kuna mambo mengi sana yanatokea pamoja na maneno
ambayo mashabiki hawawezi kuyasikia kwasababu wanakuwa mbali sana lakini
uwanjani vinatokea vitu vingi sana na ukizingatia nchi yetu sasahivi
bado haijawa kwenye teknolojia ya juu, kwasababu wenzetu hadi wakitaka
kuongea wanaziba midomo, teknolojia yao ni kubwa wanaweza kunasa kila
kitu”, ameeleza Maftah.
“Lakini kwa tukio ambalo
limetokea kwa John Bocco nadhani lilitokea na kwa Maguli pia, hata mimi
limewahi kunitokea tukio kama hilo, lakini mimi lilinitokea katika
wakati ambao nilifanya ‘action’ yani baada ya tukio kutokea mimi
nikafanya action hapohapo”.
“Nadhani yeye anajaribu kutumia
staili hiyo ili kumtoa mchezaji mchezoni lakini haangalii anapofanya
vile anakuwa amemvunjia heshima kuanzia mchezaji mwenyewe mpaka familia
yake pia”.
“Mimi sikutaka sana kufatilia
kisheria kwasababu alinifata Juma baada ya tukio lili yeye pamoja na
Haruna kwa ajili ya kuniomba msamaha kutokana na tukio lile na nikaona
atakuwa amejua makosa yake kama binadamu mimi nikaamua kumsamehe”.
“Mimi tukio lile liliniathiri
sana kwenye malengo yangu ya mpira kwasababu tokea pale hata mtu
ukiongea nane anasema huyu alimpiga mtu kichwa lakini hajui nini
kilitokea kabla ya mimi kmpiga kichwa Juma”.
“Baada ya tukio la John Bocco
kutokea liliniumiza sana natamani kama tukio langu lingeonekana kama
lilivyoonekana la Bocco, navipongeza sana vyombo vya habari kwa kuona
mambo yanayotokea uwanjani”.
“John Bocco na Juma Nyosso
nadhani ni watu wanaoongea na tayari wameshawahi kukutana kwenye timu ya
taifa, Juma anatakiwa amuombe msamaha Bocco na Bocco yeye mwenye
ataamua afanye nini mimi sitaki kuingia sana huko maana wanatakiwa
kuongea kwanza wao wawili”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni