Rais wa Ligi Kuu Hispania (LALIGA) Javier Tebas na waziri wa michezo wa Hispania Miguel Cardenal wamethibitisha kama Catalonia ikijitenga na kutoka katika umoja wa Hispania klabu ya FC Barcelona ambayo inatokea Catalonia haitashiriki Ligi Kuu Hispania.
Waziri huyo wa michezo amethibitisha kama Catalonia watajitenga na Hispania basi klabu ya FC Barcelona haitapata fursa ya kushiriki michuano ya soka ya Ulaya. Uchaguzi mkuu wa kikanda wa Catalonia unatarajia kufanyika September 27.
Catalonia wameingia katika mvutano usio rasmi na baadhi ya vyama vya siasa ambavyo vinashawishi Catalonia kujitenga na umoja wa Hispania. Hilo linaweza kutokea kama miongoni mwa vyama hivyo vitashinda viti vingi katika bunge la Catalan.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni