Sergio
Aguero, Harry Kane, Diego Costa, Alexis Sanchez, Eden Hazard na Wayne
Rooney ni wa achezaji sita waliofunga jumla ya magoli 109 kwa pamoja
msimu uliopita kwenye ligi kuu ya soka nchini England (EPL) lakini wote
wameshindwa kutamba msimu huu katika mechi ambazo tayari wameshacheza.
Mechi
sita ambazo tayari wamecheza kwenye msimu huu washambuliaji hao
wamejikuta wakifunga magoli matatu ukijumuisha idadi ya mechi zote
walizocheza hazipungui 35 wakati huo goli moja la Eden Hazard
linatazamwa kama Calum Chambers alijifunga.
Washambuliaji
wa kati Kane (Tottenham), Aguero (Manchester City) and Costa (Chelsea)
walikuwa kwenye top three ya wafungaji kwenye EPL msimu uliopita.
Sanchez (Arsenal), Hazard (Chelsea) and Rooney (Man United) walikuwa wakitokea
pembeni na wote walichangia upatikanaji wa baadhi ya magoli. Rooney
aliweka historia ya kuwa mfungaji wa muda wote wa England mwezi huu
lakini akiwa amefunga magoli manne pekee mwaka 2015.
Washambuliaji
hao wanahitaji kujiamini. Hali hiyo inaweza ikaondoka bila sababu
yoyote na kuchukua muda kurejea. Au inaweza kusababishwa na mambo
tofauti kama vile umri, malengo au wakati mwingine vyote kwa pamoja.
Makocha
wanasema huenda hali hiyo inasababishwa na mchoko (kucheza mfululizo).
Wachezaji ambao hata wao hawahisi kuchoka lakini wanaambiwa wamechoka.
Kane, Aguero and Sanchez wote walikuwa kwenye mashindano wakati ligi
ikiwa kwenye mapumziko.
Kane
alirejea nyumbani akitokea kwenye michuano ya mataifa ya Ulaya U21.
Aguero (Argentina) na Sanchez (Chile) walicheza fainali ya Copa America
Julai 4. Hawakuwepo kwenye ziara za klabu zao za kujianndaa na msimu
mpya, walianzia benchi kwenye mechi za kwanza za msimu mpya.
Aguero
ametumia muda mchache uwanjani ukilinganisha na wenzake sita lakini
amecheza mechi za kirafiki za kimataifa mapema mwezi huu nchini
Marekani, wakati Sanchez alikuwa Chile kwenye mechi dhidi ya Paraguay.
Costa,
Sanchez na Kane walikuwa ni wachezaji wapya kwenye ligi ya England
msimu uliopita na walifanya kazi kwa bidii sana. Walitumia muda mwingi
kuwasoma wapinzani wao ili kuhakikisha wanafunga magoli.
Katika
orodha ya wafungaji bora watano, wanne walikuwa ni wageni wa ligi hiyo;
Kane, Costa, Sanchez pamoja na Charlie Austin Aguero pekee ndiye hakuwa
mgeni wa ligi hiyo.
Asilimia 25 ya mashuti aliyopiga Aguero kwenye mechi sita za mwanzo msimu uliopita alifunga, lakini msimu huu ni asilimia 6.7.
Sergio Aguero
Mashuti 16 magoli 6
Mechi sita za kwanza: 2015-16
Mashuti 15 goli 1
Harry Kane
514
ni namba za dakika ambazo mshambuliaji huyo wa England amecheza
msimumhuu bila kufunga goli. Msimu uliopita alikuwa na wastani wa
kufunga kila baada ya dakika 95.
Wayne Rooney
Rooney
ameshindwa kufunga kwenye mashuti saba aliyopiga msimu huu 2015-16,
alifunga mabao matatu kwenye kila mashuti 12 aliyopiga kwenye mechi sita
za kwanza msimu uliopita.
Mechi sita za kwanza: 2014-15
Mashuti 12 magoli 3
Mechi sita za kwanza:2015-16
Mashuti 7 magoli 0
Eden Hazard
Mbelgiji
huyo wastani wake wa kupiga mashuti umeshuka msimu huu kwa mechi sita
alizocheza mpaka sasa ukilinganisha na ilivyokuwa 2014-15.
Mechi sita za kwanza: 2014-15
Asilimia 80 ya mashuti yake yalilenga goli huku yalioyokwenda nje ya lango yakiwa ni asilimia 20.
Mechi sita za kwanza 2015-16
Asilimia 50 ya mashuti yamelenga goli na asilimia 50 yameenda nje ya goli.
Diego Costa
Mechi sita magoli 8
Mechi sita za kwanza:2015-16
Mechi sita goli 1
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni