YANGA
SC imeendelea kung’ang’ania usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara kufuatia ushindi wa mabao 2-0 jioni ya leo dhidi ya wenyeji Mtibwa
Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Shukrani
kwao, wafungaji wa mabao hayo Malimi Busungu dakika ya 53 na Mzimbabwe
Donald Ngoma dakika ya 89 katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Erick
Onoka wa Arusha.
Yanga
SC sasa inafikisha pointi 15 sawa na Azam FC baada ya timu zote kucheza
mechi tano, lakini wana Jangwani wanakaa kileleni kwa wastani wao mzuri
wa mabao.
Kikosi
cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Said Mohamed, Rodgers Freddy, Issa Rashid,
Andrew Vicent, Salim Mbonde, Shabani Nditi, Vicent Barnabas, Mzamiru
Yassin, Seleman Rajab, Mohamed Ibrahim/Said Bahanuzi dk68 na Shiza
Kichuya/Jaffar Salum dk60.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvn Yondan, Said Juma 'Makapu', Malimi Busungu, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Mateo Anthony Simon dk85, Donald Ngoma na Salum Telela.
SIMBA
SC imepoza machungu ya kipigo cha 2-0 watani, Yanga SC mwishoni mwa
wiki, baada ya jioni ya leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stand
United katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Ahmada Simba wa Kagera, timu hizo zilishambuliana kwa zamu huku Hassan Dilunga wa Stand United akionyeshana ufundi na kiungo wa Simba SC, Said Ndemla katikati ya Uwanja kipindi cha kwanza.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Muingereza Dylan Kerr kipindi cha pili kupunguza idadi ya viungo wa kati na kuongeza kiungo mshambuliaji, ndiyo yaliongeza makali ya Simba SC hadi kupata bao.
Kerr
alimtoa Ndemla na kumuingiza Joseph Kimwaga mwanzoni mwa kipindi cha
pili na ni mchezaji huyo wa mkopo kutoka Azam FC ndiye aliyekwenda
kuipatia bao hilo pekee Simba SC dakika ya 57 kwa shuti kali akimalizia
krosi ya Mganda, Simon Sserunkuma.
Awali, safu ya ushambuliaji ya Simba SC iliyomtegemea Boniface Maganga pekee haikuwa tishio kutokana na Kerr kuanzisha viungo wengi, Justice Majabvi, Jonas Mkude, Pater Mwalyanzi na Ndemla.
Na
Simba SC inatimiza pointi 12 baada ya mechi tano, ikiendelea kuwa nyuma
ya Yanga SC na Azam FC ambao wameshinda kwa mara ya tano mfululizo
tangu kuanza kwa Ligi Kuu Septemba 12.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Peter Manyika, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Hassan Isihaka, Jonas Mkude, Justice Matabvi, Said Ndemla/Joseph Kimwaga dk46, Peter Mwalyanzi, Simon Sserunkuma na Boniface Maganga.
Stand United; Frank Muwonge, Nassoro Said ‘Chollo’, Abuu Ubwa, Philip Imetusela, Rajab Zahir, Hassan Dilunga, Jacob Massawe, Erick Kayombo, Vitalis Mayanja/Hassan Banda dk43, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Haroun Chanongo dk60 na Pastory Athanas.
MATOKEO MENGINE:
Azam FC 2-0 Coastal Union
Prisons 0-0 Mwadui FC
Maji maji 1-1 Ndanda FC
African Sports 0-1 Mgambo Shooting
Kagera Sugar 0-0 JKT Ruvu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni