STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 9 Oktoba 2015

BLATTER AKATA RUFANI KUPINGA KUSIMAMISHWA SIKU 90......

GAZETI la New York Times limeripoti kuwa Sepp Blatter amekata rufani rasmi dhidi kusimamishwa kwake na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. 

Blatter ambaye amekuwa rais wa FIFA toka mwaka 1998 alisimamishwa jana na kamati hiyo kwa siku tisini kufuatia uchunguzi wa kihalifu unaendelea dhidi yake. 

Taarifa ya gazeti hilo la Marekani imedai kuwa Blatter amekata rufani hiyo akidai kutotendewa haki kwani kamati haikumuita na kumuhoji kuhusiana na tuhuma zinazomkabili. 

Mawakili wa Blatter nchini Uswisi na Marekani hawakupatikana mara moja ili kutoa kauli zao kuhusiana na taarifa hizo. 

Mwanasheria Mkuu wa Uswisi amesema Septemba 25 mwaka huu walifungua ya kihalifu inayomhusu Blatter wakimtuhumu kuidhinisha kiasi cha euro milioni mbili kutoka FIFA kumuendea rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA Michel Platini pamoja na haki za matangazo za Caribbean.

Wakati huo huo;

RAIS wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki-IOC, Thomas Bach amesema FIFA lazima irejeshe uaminifu wake baada ya kufungiwa kwa Blatter, makamu wa rais Michel Platini na katibu mkuu Jerome Valcke.
 Shirikisho hilo linachunguza tuhuma za rushwa dhidi ya viongozi hao ambao wamekanusha kufanya kosa lolote.
 
Bach amesema FIFA inapaswa kutambua wakati ni sasa na hawawezi kutatua tatizo kwa kufanya uchaguzi na kuteua rais mpya pekee. 

Bach aliendelea kudai kuwa ili FIFA iweze kurejesha heshima yake inapaswa kubadili mfumo mzima ambao kwasasa unaonekana kuwa tatizo kutokana na tuhuma zilizojitokeza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox