Katika taarifa iliyotolewa jana
na klabu hiyo ilithibitisha kuwa wachezaji hao ambao walichukuliwa kwa
mkopo wanatendelea kuitumikia timu hiyo hata baada ya msimu wa 2015-2016
wa Serie A.
Dzeko na Salah walijiunga na Roma kwa mkopo wakitokea
katika klabu za Manchester City na Chelsea katika kipindi hiki cha
majira ya kiangazi.
Dzeko ambaye yuko nje kutokana na majeruhi tayari
ameshafunga bao moja toka atue jijini Rome wakati Salah yeye ameshafunga
mabao matatu na kuiacha timu hiyo ikishika nafasi ya sita katika
msimamo wa Serie A wakiwa nyuma ya vinara Fiorentina kwa alama nne.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni