Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba,
Zacharia Hans Poppe, ameibuka na kuibua hoja kuhusiana na suala la kiungo
Ramadhani Singano ‘Messi’ huku akisema hadi sasa Simba haijapokea barua ya
hukumu yake kuwa ni huru kabla hajajiunga na Azam FC.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliamua Singano kuwa mchezaji huru na baada
ya siku chache akatua Azam FC.
Lakini Hans Poppe amesema hadi jana hawakuwa
wamepata barua ya hukumu hiyo kutoka TFF kuhusiana na uamuzi huo.
“Kweli hadi leo hatuna barua, zaidi ya kusikia
na kusoma kwenye vyombo vya habari. Pamoja na hivyo, sisi tumewaandikia barua
TFF kuwaambia tunataka kujua, kwamba Simba imeonekana tumefoji mkataba, vipi
imekuwa kimya? Watupe barua na maelezo kivipi.
“Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema
angefuatilia hadi mwisho na jibu angetupatia. Vipi hadi sasa kimya?
“Kama itaendelea kuwa kimya hivi, tunaweza
kuchukua hatua nyingine za kisheria, halafu tutaonekana kama sisi ni wakorofi,
hatujafuata sheria za kimpira.
“Kama wao wapo kimya, sisi tutalipeleka
polisi na mahakamani hilo suala. Tuwashitaki kwa mtu kufoji saini, jambo ambalo
ni kinyume na sheria,” alisema Hans Poppe.
Wakati suala hilo likiendelea, kulikuwa na
lawama za figisu kwamba Messi tayari alishafanya mazungumzo na Azam FC hata
kabla ya kushinda kesi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni