MSHAMBULIAJI wa
Tottenham Hotspurs, Harry Kane anategemea wachezaji wa Liverpool kuja na
kujituma zaidi wakati watakapokutana Jumamosi hii katika Uwanja wa
White Hart Lane kwa mara ya kwanza wakiwa na meneja mpya Jurgen
Klopp.
Akiwa ametoka katika majukumu ya kimataifa na Uingereza na
wachezaji wa Liverpool akiwemo Nathaniel Clyne na Danny Ings, Kane
amesema ni jambo ambalo liko wazi kuwa wachezaji wa timu watataka
kujionyesha kwa Klopp.
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kutokana na hilo
anadhani mchezo huo utakuwa mgumu lakini watajiandaa kwa lolote
kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
Spurs haijapoteza mchezo toka
kuanza kwa msimu na wako katika nafasi ya nane, alama mbili nyuma ya
Crystal Palace walioko nafasi ya nne baada ya kuchez michezo nane.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni