MSHAMBULIAJI nyota wa
Barcelona, Neymar amesema hana shaka kuwa atakubali kusaini mkataba mpya
na mabingwa hao wa La Liga.
Wiki iliyopita katibu wa masuala ya ufundi
ya klabu hiyo Robert Fernandez alibainisha kuwa mazungumzo ya mkataba
mpya na Neymar yalikuwa yakiendelea vyema na kuongeza kuwa ana uhakika
nyota huyo atabakia Camp Nou maisha yake yote.
Nyota huyo wa kimataifa
wa Brazil, amedai mustakabali uko mikononi mwa baba yake ambaye pia ndio
wakala wake, lakini akaweka wazi kufurahia maisha katika klabu
hiyo.
Neymar amesema bado amebakisha miaka mitatu katika mkataba wake na
mambo hayo anamuachia baba yake kwani yeye jambo muhimu kwake ni
kuisaidia timu ishinde mataji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni