STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 31 Oktoba 2015

MCHEZAJI WA CHELSEA ASAKWA NA POLISI.............

 

Mchezaji wa Klabu ya Chelsea ya Uingereza anasakwa na polisi baada ya mwanamke mmoja kudai alidhulumu kijinsia.
Tayari polisi nchini Canada wametoa waranti ya kumkamata kwa makosa hayo.

Klabu ya Chelsea imekiri kuwa inafahamu kuhusu tukio hilo dhidi ya mchezaji wake Lucas Piazon.

Mchezaji huyo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 21 na ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Reading anadaiwa alikutana na mwanamke mmoja kwenye ukumbi wa disco mwezi julai.

Wawili hao walijivinjari na kujiburudisha kwa vileo na kisha wakaambatana  na kuelekea kwa nyumba moja alikoishi mwanamke huyo mjini Toronto.

Polisi nchini Canada wanadai kuwa ,Huko ndiko mchezaji huyo aliyekuwa ameambatana na mwenzake Andrey da Silva Ventura, 22 ambaye ni mlinda lango wa Brazil wanadaiwa walishindwa kujistahimili na wakamvamia kipusa huyo aliyekuwa amelala.

''waliingia ndani ya chumba chake cha kulala na kumvamia.''

''Alipoamka waliondoka na kutoweka''. ripoti ya polisi inaelezea.
Tukio hilo linaripotiwa kuwa lilitokea siku ileile ambayo mshambuliaji huyo wa Chelsea alikuwa ameifungia Brazil bao katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Panama.

Brazil ilishinda nishani ya shaba katika mashindano hayo ya Pan-Am yaliyoandaliwa Canada mwezi Julai.

Msimu huu Piazon amefunga mabao mawili katika mechi 8 alizoichezea Reading.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox