STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 3 Oktoba 2014

WENGER AKUMBUKA KICHAPO CHA 6-0 KUTOKA KWA MOURINHO.

KLABU ya Arsenal ina hamu kubwa ya kulipa kisasi kufuatia kipigo kikali walichopata kutoka kwa Chelsea machi mwaka jana, aibu ambayo meneja Arsene Wenger amekiri kuwa yeye pamoja na klabu hataweza kuisahau kamwe. Wenger atakuwa akitafuta ushindi wa kwanza kwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho kitu ambacho hajawahi kupata katika michezo mingi ya Ligi Kuu ambayo wamekutana chini ya kocha huyo Mreno. Hata hivyo Wenger anakiri kipigo cha mabao 6-0 walichopata kutoka kwa Chelsea katika Uwanja wa Stamford Bridge bado umewaachia jehara kubwa ambalo litakuwa vigumu kupona kwa haraka. Wenger amesema hawataweza kusahau kilichowatokea mwaka jana na sasa wana nafasi ya kuweka mambo sawa katika mchezo wa Jumapili. Wakiwa wametofautiana kwa alama sita na Chelsea ambao ndio vinara wa ligi hiyo, Wenger amesema ushindi ni muhimu katika mchezo huo kama wanataka kubakia katika mbio za kufukuzia taji la ligi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox