MGOMBEA urais wa
Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Prince Ali bin Hussein amepeleka rasmi
maombi yake katika kinyang’anyiro hicho, akijinasibu kurejesha heshima
ya shirikisho hilo baada ya hivi karibuni kukumbwa na kashfa za
ufisadi.
Uchaguzi huo wa kuziba nafasi ya rais aliyesimamishwa Sepp
Blatter ulipangwa kufanyika Februari mwakani, ingawa mkutano wa dharura
unaotarajiwa kuitishwa baadae mwezi huu unaweza kusogeza muda huo
mbele.
Taarifa zinadai kucheleshwa kwa uchaguzi kutatokana na
kusimamishwa kwa siku tisini kwa Blatter na rais wa Shirikisho la Soka
la Ulaya-UEFA, Michel Platini ingawa wote wamekanusha kufanya jambo
lolote baya.
Hata hivyo, Prince Ali, ambaye alishindwa na Blatter katika
uchaguzi wa Mei kabla ya ris huyo kutangaza kujiuzulu aliwasilisha
barua yake kwa wajumbe wa mashirikisho akiomba ridhaa yao ili aweze
kuitoa FIFA katika wingu zito walilopo hivi sasa.
Prince Ali amesema
hawataweza kubadili yaliyotokea lakini ana uhakika FIFA inaweza kuwa na
mustakabali mzuri wa baadae kwa kurejesha maadili na heshima yake ya
awali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni