NCHI kadhaa zinatarajiwa
kujitoa kumuunga mkono Michel Platini katika harakati zake za kutafuta
nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kama hatatoa maelezo
ya uhakika juu ya paundi milioni 1.35 alizolipwa na Sepp Blatter.
Rais
huyo wa FIFA yuko chini ya uchunguzi wa kihalifu kuhusiana na malipo
hayo yaliyofanywa mwaka 2011, wakati Platini ambaye ni rais wa
Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA akihojiwa kuhusiana na hilo. Wote
wawili Blatter na Platini wamekanusha kufanya kosa lolote baya.
Wajumbe
54 kutoka Vyama vya Soka vya nchi za Ulaya wanatarajiwa kukutana na
shirikisho hilo leo nchini Uswisi kujadili suala hilo.
Kukosekana kwa
mkataba wa maandishi kutokana na malipo hayo kumesababisha nchi kadhaa
kufikiria uamuzi wao wa kumuunga mkono Platini katika uchaguzi huo
utakaofanyika Februari mwakani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni