KLABU ya Manchester City
ambao walifungiwa mwaka jana na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA kwa
kukiuka sheri ya matumizi, wametoa faida ya mwaka kwa mara ya kwanza
toka timu hiyo iliponunuliwa na Sheikh Mansour bin Zayed mwaka
2008.
Klabu hiyo ya Ligi Kuu ilitoa taarifa yake ya mwaka kwa msimu wa
2014-2015 jana. Taarifa hiyo iliyotolewa imeonyesha kuwa klabu hiyo
imepata faida ya paundi milioni 10.7 huku mapato yake kwa mwaka
yakipanda na kufikia rekodi ya paundi milioni 352.
Taarifa hiyo
iliyotolewa na mwenyekiti wake Khaldoom Al Mubarak iliendelea kudai kuwa
sasa City imeanza kuingiza faida huku wakiwa hawana deni lolote.
Mwaka
jana klabu hiyo ilitozwa faini ya paundi milioni 60 kwa kukiuka sheria
hiyo ya UEFA huku pia kikosi chao kikipunguzwa kwa ajili ya michuano ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni