BODI ya misamaha nchini
Afrika Kusini imedai kuwa mwanariadha nyota mlemavu wa nchi hiyo, Oscar
Pistorius ataachiwa kutoka gerezani na kwenda kutumikia kifungo cha nje
Jumanne ijayo.
Pistorius alifungwa miaka mitano jela mwaka jana baada ya
kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia.
Mwanariadha huyo alimfyatulia
risasi na kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kupitia mlango wa bafuni
akidhania kuwa ni mwizi aliyevamia nyumbani kwake.
Waendesha mashitaka
wamekata rufani, wakidai kuwa Pistorius alipaswa kuhukumiwa kwa kosa la
mauaji na kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Novemba 3 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni