MEI 7, mwaka huu msimu wa 2015/16 unatarajiwa kufikia tamati kwa timu zote 16 kushuka viwanjani katika mikoa tofauti, hiyo itakuwa ni baada ya mikikimikiki ya takribani miezi nane tangu msimu ulipoanza Septemba 12, mwaka jana.
Ligi hiyo ambayo kwa sasa inaongozwa na Simba, inazishirikisha timu 16, na baada ya msimu kumalizika timu tatu zitashuka daraja huku tatu kutoka Ligi Daraja la Kwanza zikija kuziba nafasi zao kwa ajili ya msimu ujao.
Takribani
mechi saba mpaka kumi zimebaki kwa timu zote kukamilisha msimu, lakini mpaka
sasa hakuna timu iliyojihakikishia ubingwa wala zile zitakazoshuka
hazijajulikana rasmi licha ya kuwepo zinazotajwa kuwa kwenye hatari ya kushuka
kwa jinsi mwenendo wao ulivyo.
Vita ya kuwania ubingwa mpaka sasa ipo kwa timu tatu, Simba, Yanga na Azam ambazo ndizo zimepishana pointi chache tofauti na ile inayofuata baada ya hizo.
Simba ipo kileleni na pointi zao 54, hiyo ni
baada ya kucheza mbili zaidi ya Azam na Yanga. Katika michuano mbalimbali, kila
timu huwa inaringia uwanja wake wa nyumbani inaoutumia kwa mechi zake, katika
mechi saba zilizobaki za Simba, nne watacheza nyumbani na tatu pekee
watalazimika kwenda ugenini.
Tunapozungumzia viwanja vya nyumbani kwa timu hizi
tatu, tunamaanisha Uwanja wa Taifa unaotumiwa na Yanga na Simba na Uwanja wa
Azam Complex ambao Azam FC huutumia kwa mechi zao za nyumbani, lakini
inapocheza na Yanga au Simba, wanalazimika kwenda Taifa na kuonekana kama wapo
ugenini japo ratiba inaonyesha wao ndiyo wapo nyumbani.
Yanga nayo mechi zao
tisa zilizobaki, nne pekee watacheza nyumbani na tano ugenini huku Azam mechi
zao tisa, nne watacheza nyumbani na tano ugenini.
Katika hesabu zilizofanywa na
mchambuzi wa makala hii na kama zikienda sawia, bila shaka bingwa wa msimu huu
tayari kashajulikana.
Simba Ilianza vizuri msimu huu kwa kushinda mechi mbili
mfululizo ugenini kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ambapo awali palionekana
kuwa kikwazo kwao, lakini ikiwa chini ya Muingereza aliyetimuliwa kikosini
hapo, Dylan Kerr wakaweza kuondoka na pointi zote sita kwenye mechi zao mbili
walizocheza uwanjani hapo, dhidi ya JKT Mgambo na African Sports.
Hakuna
asiyefahamu kama ukienda ugenini lazima upate shida kuondoka na pointi, lakini
ukiangalia rekodi ya Simba msimu huu, imeshinda ugenini mechi sita kati ya
tisa, sare moja na imefungwa mbili.
Kumbuka imebakiwa na mechi tatu ugenini,
dhidi ya Coastal Union, Majimaji na Mtibwa.
Kwa jinsi mechi hizo zilivyo,
wanaweza wasipate kikwazo sana watakapocheza na Majimaji, lakini hizo zingine
kupata pointi ni nusu kwa nusu.
Ukiachana na mechi za nje ya Dar, Simba
imecheza mechi 14 ndani ya Uwanja wa Taifa, imeshinda 11, sare moja dhidi ya
Azam na imepoteza mbili ambazo zote ni dhidi ya Yanga huku bado ikiwa
haijacheza tena na Azam uwanjani hapo.
Yanga Inashika nafasi ya pili kwa sasa
ikiwa na pointi 50, imebakiwa na michezo tisa kabla ya kuhitimishwa kwa ligi.
Ikifanikiwa kushinda mechi zake mbili ili kuwa sawa na Simba kimichezo
itafikisha pointi 56, inaweza kukaa kileleni kutokana na kuwa na wastani mzuri
wa mabao.
Katika mechi zake 21 ilizocheza mpaka sasa, 14 imechezea nyumbani na
saba ugenini.
Katika hizo, nyumbani imeshinda 12, sare mbili ambazo zote ni
dhidi ya Azam. Ikiwa ugenini, imeshinda tatu, sare tatu na imepoteza moja.
Katika mechi zilizobaki itaenda ugenini mara tano. Kikwazo kwao kinaweza kuwa
kwa Ndanda na Mbeya City kutokana na rekodi yao huko nyuma, lakini kwa timu
zingine za Majimaji, Stand United na Toto African inaweza isikumbane na
changamoto kubwa sana kwa jinsi rekodi yao inavyosema inapocheza huko.
Nyumbani
imebakisha mechi nne, ukiziangalia kwa jicho la mbali hakuna itakayoweza
kuinyima Yanga pointi ukizingatia kwamba mpaka sasa haijapoteza nyumbani.
Mtibwa, Kagera, Mgambo na Mwadui ndizo itacheza nazo nyumbani.
Azam Mechi zake
tisa zimebaki kumaliza msimu. Inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 50,
endapo itashinda mechi zake mbili ili kuwa sawa na Simba kimichezo, itafikisha
pointi 56 sawa na Yanga kama nayo itachanga vizuri karata zao kwa viporo vyao,
hapo watakuwa wanaiacha Simba kwa pointi mbili.
Azam italazimika kusafiri
kutoka nyumbani kwao kwenda ugenini mara tano kama ilivyo kwa Yanga. Katika
mechi 21, Azam imecheza tisa nyumbani na kushinda nane, sare moja huku ikiwa
haijapoteza hata mchezo mmoja.
Kwa michezo ya ugenini, imecheza 12, imeshinda
saba, sare nne na imepoteza mmoja.
Katika mechi za nyumbani zilizobaki haiwezi
kupata shida sana kwenye kusaka ushindi, lakini wanapaswa kuwa makini na
Mgambo.
Zingine ambazo ni Ndanda, Stand, JKT Ruvu na Majimaji uwezo wa kushinda
ni asilimia 70. Ugenini, itakumbana na Simba na Mtibwa, hizi ndizo mechi ngumu
kwao, lakini zilizobaki dhidi ya Toto African, African Sports na Kagera Sugar
si kikwazo sana kwao.
Hitimisho Kutokana na takwimu hizo
na jinsi mechi za ugenini zilivyokuwa ngumu, tumebaini kwamba zote zina mechi
mbili ngumu huko, ni jukumu lao kuzichanga vyema karata zao ili kuepuka majanga
ya kudondosha pointi, kama moja ikiteleza basi inaweza kuwa ndiyo basi tena
katika mbio za kuwania ubingwa, lakini kama zote zitakaza na kupata matokeo
mazuri, bila shaka Yanga ndiyo inayo nafasi kubwa ya kuwa bingwa, Azam ya pili
na Simba ya tatu.
Hakuna aijuaye kesho, tusubiri tuone mwisho wake.
Mechi zilizobaki kwa Yanga;
Yanga Vs Mtibwa Taifa
Toto Vs Yanga Kirumba
Yanga Vs Mwadui Taifa
Yanga Vs Kagera Taifa
Stand Vs Yanga Kambarage
Yanga Vs Mgambo Taifa
Mbeya City Vs Yanga Sokoine
Ndanda Vs Yanga Nangwanda
Majimaji Vs Yanga Majimaji
Mechi zilizobaki kwa Azam;
Mtibwa Vs Azam Manungu
Azam Vs Ndanda Azam Complex
Azam Vs Stand Azam Complex
Azam Vs JKT Ruvu Azam Complex
Toto Vs Azam Kirumba
Azam Vs Majimaji Azam Complex
Simba Vs Azam Taifa
Kagera Vs Azam Mwinyi
African Sports Vs Azam Mkwakwani
Azam Vs Mgambo Azam Complex
Mechi zilizobaki kwa Simba;
Coastal Vs Simba Mkwakwani
Majimaji Vs Simba Majimaji
Simba Vs Toto Taifa
Simba Vs Azam Taifa
Simba Vs Mwadui Taifa
Mtibwa Vs Simba Jamhuri
Simba Vs JKT Ruvu Taifa
Hakuna aijuaye kesho, tusubiri tuone mwisho wake.
Mechi zilizobaki kwa Yanga;
Yanga Vs Mtibwa Taifa
Toto Vs Yanga Kirumba
Yanga Vs Mwadui Taifa
Yanga Vs Kagera Taifa
Stand Vs Yanga Kambarage
Yanga Vs Mgambo Taifa
Mbeya City Vs Yanga Sokoine
Ndanda Vs Yanga Nangwanda
Majimaji Vs Yanga Majimaji
Mechi zilizobaki kwa Azam;
Mtibwa Vs Azam Manungu
Azam Vs Ndanda Azam Complex
Azam Vs Stand Azam Complex
Azam Vs JKT Ruvu Azam Complex
Toto Vs Azam Kirumba
Azam Vs Majimaji Azam Complex
Simba Vs Azam Taifa
Kagera Vs Azam Mwinyi
African Sports Vs Azam Mkwakwani
Azam Vs Mgambo Azam Complex
Mechi zilizobaki kwa Simba;
Coastal Vs Simba Mkwakwani
Majimaji Vs Simba Majimaji
Simba Vs Toto Taifa
Simba Vs Azam Taifa
Simba Vs Mwadui Taifa
Mtibwa Vs Simba Jamhuri
Simba Vs JKT Ruvu Taifa
www.mdosejr@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni