STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 3 Aprili 2016

BBC WAIPOTEZA KABISAAA MSN KWENYE EL CLASICO, CR7 SHUJAA....


Bale posted this picture of the victorious Real squad following their 2-1 victory against Barca at the Nou Camp 
Ilikuwa ni Clasico ya namna tofauti na historia.

Barcelona walishindwa kuimudu timu ya Real Madrid ambayo ipo kwenye njia panda ya maendeleo chini ya Zidane.

Barca Blaugrana walishindwa kucheza kwa mfumo wao na ufundi uliojengwa na Luis Enrique, walishindwa kuwasha moto wao wa siku zote. Madrid walikamilisha kazi, lakini haikuwa kazi rahisi.
 Barca star Lionel Messi shakes hands with Real Madrid forward Cristiano Ronaldo as the pair get ready for El Clasico 
Sergio Ramos alionywa mara kadhaa kabla ya kuoneshwa kadi nyekundu. 

Lakini nyota wa Barcelona hawakukata tamaa, walipambana kusaka bao hadi walipopata goli la kwanza kupitia Gerard Pique.
 Real Madrid manager Zinedine Zidane (left) and Barca boss Luis Enrique shouts instructions from the sideline 
Barca waliendeleza falsafa yao ingawa walizidiwa kwa namna fulani - Johan Cruyff - ambaye alikumbukwa muda wote wa mechi - asingefurahishwa na Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar kushindwa kufunga.

Suarez hakuwa katika ubora wake wa siku zote; Neymar hakuweza kupiga hata shuti moja golini; Messi pamoja na uwezo wake mkubwa hakuweza kuzifumania nyavu - hivyo Barca wakapata goli kupitia Gerard Pique.
Barca keeper Claudio Bravo rises high to claim a corner as both sides chased a breakthrough goal Haikuwa Clasico ya wachezaji fulani nyota kama ilivyo siku zote, timu zote zilicheza kwa kujituma, baada ya Karim Benzema kutupia, hadi mabeki wa Real Madrid walionyesha kuamka zaidi.

Jambo mojawapo ambalo lingeweza kuamsha tabasamu la Cruyff ni kuingia kwa Arda Turan kuchukua nafasi ya Ivan Rakitic kipindi cha pili. Luis Enrique alionesha ujasiri kumuingiza Mturuki huyo kufanya jukumu muhimu dimbani. Hawezi kucheza katika kiwango kikubwa kama cha Rakitic lakini ni mtu asiyetabirika.
 The capacity crowd packed into the Nou Camp unveil a mosaic tribute to former Barcelona player and manager Johan Cruyff before kick-off
Lakini kwa bahati mbaya, mabadiliko hayo hayakuzaa matunda yaliyotarajiwa. Uamuzi wake hakulipa hata baada ya kutolewa kwa Sergio Ramos dakika saba zikiwa zimesalia. Kwa mara ya kwanza Madrid na si Barca walikuwa na ari njema.
 
Dakika za majeruhi mashabiki wa Los Blancos walinyanyuka vitini kushangilia bao safi kabisa la ushindi kutoka kwa Cristiano Ronaldo, aliyefunga kwa pasi nzuri kutoka kwa Gareth Bale, Lo! zawadi iliyoje kutoka kwa nyota huyo raia wa Wales?

Zinedine Zidane ameonyesha ufundi wake kwa kushinda mechi yake ya kwanza El Clasico, Ni dhahiri kikosi cha Real Madrid kimeonyesha mabadiliko ya hali ya juu sana.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox