STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 2 Aprili 2016

TFF YAUGWAYA KWA YANGA SASA MCHEZO DHIDI YA MTIBWA WASOGEZWA MBELE.......

 
SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limekubali kuisogeza mbele mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya mabingwa watetezi, Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar iliokuwa ichezwe Jumatano (Aprili 6, 2016) na badala yake itapigwa Aprili 16 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
   
Hiyo inafuatia malalamiko ya Yanga kupangiwa mechi tatu ndani ya wiki moja kabla ya kumenyana na Al Ahly ya Misri Jumamosi ijayo katika Ligi ya Mabingwa Afrika. 
  Maana yake, Yanga SC watashuka dimbani leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Kagera Sugar ya Bukoba katika mfululizo wa Ligi Kuu na baada ya hapo watakwenda kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Ahly mwishoni mwa wiki.
   
Akizungumza na chombo kimoja cha habari leo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Murro amesema kwamba mechi hiyo imeondolewa na badala yake itachezwa Aprili 16, kama ilivyopangiwa na Shirikisho hilo.
  Alisema kwa matokeo hayo, kikosi hicho baada ya mchezo wa  dhidi ya Kagera Sugar, wataendelea kujifua kujiandaa na mechi dhidi ya Al Ahly iliyopangwa kufanyika Aprili 9 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kwa upande wake, Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema wao wamekataa kuahirishiwa mchezo wao na Ndanda FC na watashuka dimbani Aprili 6 kumalizia kiporo hicho.

CHANZO;BIN ZUBEIRY

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox