Katika hatua nyingine kamati pia imeipiga faini ya shilingi milioni mbili timu ya Coastal baada ya mashabiki wa timu hiyo kufanya vurugu
Kamati pia baada ya kupitia ripoti ya kamisaa wa ule mchezo ikaamua kumfungia mwaka mmoja muamuzi Abdallah Kambuzi kwa kuonekana kutoumudu mchezo hali iliyopelekea amani kutoweka uwanjani na muamuzi msaidizi namba mbili Charles Simon akiondolewa kwenye orodha ya waamuzi
Kwa maana hiyo sasa ni rasmi mchezo wa fainali kwenye kombe la ASFC itazikutanisha timu kutoka Dar kati ya Yanga dhidi ya Azam ni lazima mmoja wapo ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa mwakani


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni