STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 12 Aprili 2016

HII HAPA RATIBA YA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO, YANGA KUVAANA NA "WAARABU WA TANGA"

YANGA SC itamenyana na Coastal Union katika Nusu Fainali ya michuano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federations Cup 2016.

Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga Aprili 24, mwaka huu, siku ambayo Azam FC itamenyana na Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Tanga Aprili 24, mwaka huu pia. 
 
Hiyo inafuatia droo iliyopangwa jana studio za Azam TV, wadhamini wa michuano hiyo, Tabata, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa.
 
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, Esther Chabruma ndiye aliyechagua timu za kumenyana katika Nusu Fainali katika droo hiyo, akisimamiwa na Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto.
 
Coastal Union iliingia Nusu Fainali baada ya kuitoa Simba SC kwa kuifunga mabao 2-1, wakati Azam FC iliitoa Prisons kwa kuifunga 3-1, Mwadui FC iliitoa Geita Gold kwa kufunga 3-0 na Yanga SC iliwafunga Ndanda FC 2-1.
 
Bingwa wa Kombe la ASFC, michuano iliyoanza na timu 64 Novemba mwaka jana, ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
 
Katika hatua ya awali, kila timu ilipatiwa fedha za usafiri Sh Milioni 3, na vifaa vya mashindano kutoka kwa wadhamini, Azam TV ikiwa ni sehemu ya udhamini wa Bilioni 3.3.
 
Bingwa wa Kombe la ASFC atajinyakuliwa kitita cha Sh. Milioni 50,
Fainali inatarajiwa kuchezwa wiki moja baada ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika.
 
Mara ya mwisho michuano hiyo ilifanyika mwaka 2002 na JKT Ruvu ikaifunga Baker Rangers ya Magomeni katika fainali, wakati ikijulikana kama Kombe la FAT (Chama cha Soka Tanzania).

ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO
1967    Yanga SC 
1974    Yanga SC
1985    Maji Maji
1995    Simba SC
1996    Sigara
1997    Tanzania Stars
1998    Tanzania Stars
1999    Yanga SC
2000    Mtibwa Sugar
2001    Yanga SC 
2002    JKT Ruvu  


Chanzo: Bin Zubeir

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox