STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 13 Aprili 2016

NIYONZIMA AKIWEKA KWENYE "FRIJI" KIPORO CHA YANGA, AZAM WAITAMBIA MTIBWA MANUNGU

Goli safi la Haruna Niyonzima limeipa pointi tatu muhimu mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Yanga SC mbele ya vijana wa Jamhuri Kihwelo Julio Mwadui FC mchezo uliocezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo wa leo uliotawaliwa kila aina ya ufundi, Yanga SC waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 2 ya mchezo kupitia kwa Saimon Msuva.

Kuingia kwa goli hilo kuliwafanywa Mwadui kucheza kwa tahadhari kubwa, na kujaribu kupandisha mashambulizi kadha langoni mwa yanga sc, huku yanga wakiendeleza kasi yao.

Katika dakika ya 13 Kelvin Sabato aliisawazisha Mwadui FC na kupeleka mchezo kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.

Kipnid cha pili kilianza kwa kasi, huku yanga wakimuingiza beki Vicent Bosue kuchukuwa nafasi ya Pato Ngonyani, kitendo kilichoimarisha safu yao ya ulinzi.

Katika dakika 67 beki wa Mwadui FC Sabo alizawadiwa kadi nyekundu na kupelekea Mwadui FC kumaliza mchezo wakiwa pungufu.

Yanga SC walitumia upungufu huo na kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa Mwamdui FC, lakini uimara wa Shaban Kado uliwapeleka yanga sc kungoja mpaka katika dakika ya 86.

Alikuwa Haruna Niyonzima akimalizia klwa ustadi mpira wa urejesho toka kwa Donald Ngoma aliyeunga krosi ya Oscar Joshua na kuiandikia Yanga goli la pili na kupeleka mchezo kumalizka kwa yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

Kwa matokeo hayo ya leo Yanga SC wanafikisha pointi 56 baada ya kucheza michezo 23 wakiwa nyuma kwa mchezo mmoja dhidi ya vinara Simba SC wanoangoza ligi kwa tofauti ya pointi 1.

Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Pato Ngonyani/Vincent Bossou dk46, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe/Malimi Busungu dk79 na Issoufour Boubacar/Godfrey Mwashiuya dk46.  
Mwadui FC: Shaaban Kado, Malika Ndeule, David Luhende, Iddy Mobby, Joram Mgeveke/Abdallah Mfuko dk30, Anthony Mataogolo, Jabir Aziz, Razack Khalifan, Kevin Sabati, Juma Mnyate na Hassan Kabunda/Nizar Khalfan dk57.
 
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Azam FC imeshinda 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
 
Shukrani kwake, Nahodha John Raphael Bocco aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 62 kwa penalti baada ya mshambuliaji Kipre Herman Tchetche kuchezewa rafu kwenye boksi.
 
AzamFC sasa inafikisha pointi 55 baada ya kucheza mechi 24, ikiendelea kukaa nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na Simba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox