KLABU ya Paris
Saint-Germain-PSG inadaiwa kuwa katika mazungumzo na meneja wa zamani wa
Chelsea, Jose Mourinho.
PSG tayari wameshanyakuwa taji la La Liga msimu
huu na wako katika nafasi nzuri ya kutwaa taji la Kombe la Ligi na
Kombe la Ufaransa, hata hivyo lengo lao kubwa lilikuwa ni kuvuka hatua
ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kufuatia
kuenguliwa katika michuano hiyo ya Ulaya na Manchester City, meneja wa
klabu hiyo Laurent Blanc amekuwa katika hatari ya kutimuliwa kufuatia
taarifa hizo.
Mourinho amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda
Manchester United kwa kipindi kirefu lakini uwezekano wa timu hiyo
kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao unaweza kumfanya
Louis van Gaal kuendelea na kibarua chake.
PSG walipotafutwa kutoa kauli
yao kuhusiana na taarifa hizo walikataa kusema chochote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni