STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 30 Juni 2016

FAHAMU YOTE YA KIMICHEZO BARANI ULAYA NA AMERICA ................


CHILE KUCHEZA NA MABINGWA WA EURO 2016.

MABINGWA wa michuano ya Copa America, Chile wanatarajiwa kupambana na bingwa wa michuano ya Ulaya anakayepatikana baadae mwezi ujao.
 
 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na rais wa Shirikisho la Soka la America Kusini-CONMEBOL, Alejandro Dominguez, mchezo huo utakaokutanisha bingwa wa Copa America na Euro 2016 utachezwa katika miezi michache ijayo.
 
 Wakati Chile wakijihakikishia nafasi yao ya kushiriki Kombe la Shirikisho mwaka 2017, Dominguez amebainisha kuwa tayari wameshatuma barua ya maombi ya mchezo huo kwa Shirikisho la Soka la Ulaya. 
 
Dominguez amesema mara baada ya kutuma barua hiyo wamepata majibu ya matumaini kwamba mchezo huo unaweza kuwepo hivyo wanachotakiwa kufanya ni kutafuta tarehe itakayofaa.
 

HULK AKAMILISHA USAJILI WAKE CHINA.

KLABU ya Shanghai SIPG imekamilisha rasmi usajili wa nyota wa kimataifa wa Brazil, Hulk kutoka klabu ya Zenit St Petersburg ya Urusi. 
 
Klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya China-CLS imelipa kitita cha euro milioni 56 kwa mchezaji huyo ambachi kimeweka rekodi mpya ya usajili katika ligi hiyo.
 
 Zenit pia wanatarajiwa kupata bakshishi ya euro milioni mbili zaidi kama mshambuliaji huyo atafunga mabao zaidi ya 15. 
 
Inadaiwa kuwa Hulk amekubalia mshahara wa euro milioni 12.5 kabla ya bakshishi, kiasi ambacho kitamfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi CLS. 
 
Klabu hiyo ilithibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wake na kudai kuwa Hulk alisaini mkataba wake pindi alipomaliza vipimo vyake vya afya.
 
 

SCOLARI ATAMANI KUINOA UINGEREZA.

KOCHA wa zamani wa Brazil, Luiz Felipe Scolari ametangaza nia yake ya kuja kuwa meneja ajaye wa timu ya taifa ya Uingereza. 
 
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 67 ambaye aliiongoza Brazil kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2002, alipata nafasi ya kuchukua mikoba ya Sven-Goran Eriksson kama meneja wa Uingereza mwaka 2006 kabla ya kujitoa kutokana na kushambuliwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo. 
 
Scolari ambaye alishindwa kupata mafanikio katika klabu ya Chelsea kwa kutimuliwa baada ya miezi sita, amesisitiza kuwa yuko tayari kwa chochote ambacho Chama cha Soka Uingereza kitahitaji kutoka kwake kama akiteuliwa kuwa kocha. 
 
Akihojiwa Scolari amesema kwasasa yeye bado ni meneja wa Guanghou na anakipenda kibarua chake lakini anafahamu umuhimu wa kibarua cha kuinoa Uingereza katika ulimwengu wa soka hivi sasa.
 
 Kocha huyo aliendelea kudai kuwa anahusudu soka la Uingereza na anafahamu mahitaji ya timu ya taifa kuwa inahitaji mafanikio.
 
 

SIMEONE ASISITIZA KUENDELEA KUBAKIA ATLETICO.

MENEJA wa Atletico Madrid, Diego Simeone amefafanua kauli yake aliyoitoa kufuatia timu yake kupoteza mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi uliopita.
 
 Atletico ilishindwa kutamba kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu baada ya kutandikwa tena mahasimu wao wa jiji Real Madrid. 
 
Baada ya mchezo huo ambao walipoteza kwa changamoto ya mikwaju ya penati jijini Milan, Simeone amesema anatarajiwa kuchukua muda kufikiria kuhusu mustakabali wake katika klabu hiyo. 
 
Lakini meneja huyo mwenye umri wa miaka 46 amesema kauli hiyo aliitoa wakati akiwa katika kipindi kibaya, kwani hana mpango wowote wa kuondoka Atletico kwasasa. 
 
Simeone aliendelea kudai kuwa Atletico itaendelea kuwa moja ya vikosi bora kabisa katika ulimwengu wa soka katika miaka mingi ijayo. 
 
Meneja huyo amesema timu pekee zinazowazidi kwa ubora ni Barcelona, Real Madrid na Bayern Munich, hakuna nyingine.
 
 

                                            NOLITO ANUKIA CITY.

WINGA mahiri wa kimataifa wa Hispania, Nolito anadaiwa kuwa tayari ameshatua jijini Manchester kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Manchester City. 
 
Nyota huyo anatarajiwa kuwa mchezaji wa pili kusajili na meneja mpya wa klabu hiyo Pep Guardiola baada ya kufikia makubaliano mabo binafsi na timu hiyo ya Ligi Kuu.
 
 Nolito anatarajiwa kumalizia baadhi vitu vichache vilivyobaki katika uhamisho wake kutoka Celta Vigo ambao umegharimu kiasi cha paundi milioni 14, pindi atakapotembelea kituo cha michezo cha City. 
 
Mara baada ya kukamilisha vipimo vyake vya afya, Nolito anatarajiwa kutembezwa katika kituo hicho kabla ya kupigwa picha na kutambulishwa rasmi kwa vyombo vya habari. 
 
Nyota huyo atakuwa mchzaji pili kusajiliwa na City baada ya Ilkay Gundogan aliyesajiliwa kutokea Borussia Dortmund Juni 2 mwaka huu.
NEYMAR KUJITIA KITANZI BARCELONA. RAIS wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amesema Neymar anatarajiwa kusaini mkataba mpya katika kipindi cha siku chache zijazo. Mkataba wa sasa wa neymar unamalizika Juni mwaka 2018 na mazungumzo ya mkataba mpya yamekuwa yakindelea kwa muda sasa hivyo kuzusha tetesi kuwa klabu za Real Madrid, Paris Saint-Germain au Manchester United zinaweza kulipa kitenzi cha euro milioni 200 kilichowekwa katika mkataba wake. Hata hivyo, akiongeza na wanahabari mapema leo, Bartomeu amesema Neymar hatakwenda popote na katika siku chache zijazo atasaini mkataba mpya wa miaka mitano zaidi. Wakala wa zamani wa Neymar, Wagner Ribeiro hivi karibuni alidai kuwa kuna klabu tatu kubwa zinazomfukuzia nyota huyo wa kimataifa wa Brazil lakini mwenyewe anafurahia kuendelea kubakia Camp Nou. Neymar alijiunga na Barcelona akitokea Santos mwaka 2013 a kufanikiwa kushinda taji la La Liga na Kombe la Mfalme mara mbili pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka jana.

Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox