STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 1 Julai 2016

HABARI ZOTE KUBWA ZA KIMICHEZTO TANZANIA........

 

KOCHA Mcameroon, Joseph Marius Omog leo amesaini Mkataba wa miaka miwili kufundisha Simba SC na amesema atarejesha furaha ya mataji Msimbazi.
 
Omog amesaini mchana wa leo katika hoteli ya Regency, Mikocheni, Dar es Salaam mbele ya Rais wa klabu, Evans Elieza Aveva na akasema sera yake ni ushindi na mataji.

 
“Nimefurahi kusaini Mkataba wa kufanya kazi Simba SC, ni klabu kubwa na ninaamini kwa ushirikiano wa pamoja na uongozi, wanachama na wachezaji tunaweza kufanikiwa,”amesema Omog aliyewasili usiku wa kuamkia leo.

 

Rais wa Simba SC, Evans Aveva (katikati) akimkabidhi jezi ya klabu hiyo kocha Omog baada ya kusaini Mkataba. Kulia ni Katibu Mkuu, Patrick Kehemele
Omog (katikati) akiupitia Mkataba kabla ya kusaini. Kulia ni Rais Aveva na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Collin Frisch

Simba inakuwa klabu ya pili kwa Omog kufundisha Tanzania baada ya awali kuwa na Azam FC, aliyoiongoza kwa msimu mmoja na nusu ikishinda mechi 30 kati ya 55 za mashindano yote, sare 14 na kufungwa 11.
 
Mwalimu huyo aliyeipa Leopard FC ya Kongo Brazaville Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2014, enzi zake alichezea Yaounde na ni mwalimu wa kiwango cha juu cha ufundishaji soka na mazoezi ya viungo aliyehitimu vizuri mafunzo yake katika Chuo cha Vijana na Michezo, INJS mjini Yaounde, Cameroon. 

 
Alikwenda kujiendeleza kielimu nchini Ujerumani na kwa pamoja na Pierre Njili na Martin Ndtoungou walipata Stashahada za ukocha na leseni za UEFA daraja la B mwaka 1987. 

 
Aliporejea nchini mwake, Joseph Marius Omog, alifundisha timu kadhaa kama Fovu ya Baham na Aigle ya Menoua na akazifikisha fainali ya Kombe la Cameroon klabu zote. 

 
Mwaka 2001 aliteuliwa kuwa Msaidizi wa kocha Mjerumani, Winfried Schafer katika timu ya taifa ya Cameroon, Simba Wasiofungika chini ya Nahodha Samuel Eto’o haswa kutokana na kujua kwake Kijerumani, kwa sababu kocha huyo alikuwa hazungumzi Kiingereza wala Kifaransa, lugha zinazotumika nchini humo. 

 
Mwaka 2003 aliteuliwa kuwa kocha Mkuu wa timu ya taifa baada kuondoka kwa Winfried Schafer, lakini akafukuzwa mwaka 2010 kutokana na matokeo mabaya na kushindwa kuiwezesha Cameroon kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika.

 
Akaamua kutoka nje ya nchi na mwaka 2011 alijiunga na AC Leopard ya Kongo, ambayo aliiwezesha kutwaa Kombe mwaka huo huo na kuipa tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho. 

 
Na akafanikiwa kuiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe hilo la Afrika mwaka 2012 kwa kuifunga Djoliba ya Mali mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano na kutengeneza ushindi wa jumla wa 4-3. Mwaka 2014 alijiunga na Azam FC ambayo aliipa taji la kwanza la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa msimu.  

 
Je, mafanikio hayo atayahamishia Simba? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.


WAKATI HUO;

 
Mdhamini wa Klabu ya Simba, Ramesh Patel akipokea hati ya Kiwanja cha Bunju Plot no 226 Block 1 kutoka kwa Ofisa wa Ofisi ya Msajili wa Hati, Mpoki Mwalufunda na anayeshuhudia kwa nyuma ni Msajili Msaidizi wa Hati, Apollo Laizer.

Sasa Simba inaweza kuanza ujenzi wa uwanja wake wa mazoezi wakati wowote ule kwa kuwa jambo hilo ndiyo lilikuwa likiwakwamisha.

Taarifa za ndani zinaeleza, Simba walilazimika kusubiri hadi watakapopata hati hiyo ili waanze kazi ya ujenzi ambayo kama wangepata hati hiyo, wangeweza kuanza mwaka jana.

TAARIFA NYINGINE KUBWA;

MKUU wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Jerry Muro ameutaka uongozi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kumuomba radhi kwa kumdhalilisha baada ya kumuandikia barua ya malalamiko ya kumtaka kwenda kwenye kamati ya maadili.

Akiongea kwa masikitiko mbele ya waandishi wa Habari katika makao makuu ya klabu hiyo, Jerry alisema kuwa TFF walipaswa kuwaandikia barua Yanga ambao ndio mwanachama wao na si yeye kwa mujibu wa katiba ya nchi.

TFF ilitoa tamko jana kupitia kwa Ofisa Habari wake Alfred Lucas ya kumuita Jerry mbele ya kamati ya maadili ya shirikisho hilo kutokana na maneno ya kichochezi aliyoyatoa mbele ya waandishi wa Habari siku chache zilizopita.

"Mimi sio mwanachama wa TFF, nimeajiriwa na Yanga kwahiyo kama kuna nililofanya ilibidi waiandikie klabu sio mimi, ila itajulikana mbivu na mbichi," alisema Jerry.

Jerry anatakiwa kufika mbele ya kamati hiyo kesho Julai 2 katika ofisi za TFF saa 4 asubuhi kwa ajili ya kusikiliza shauli hilo ambalo alisema atafika bila kukosa.

"Wapenzi na wanachama wa Yanga wamekuwa wakiniuliza kuwa nitahudhuria au la, kiukweli kesho nitaenda kuwasikiliza wanachotaka ili ijulikane mbivu na mbichi" alisema Jerry.

Aidha Jerry aliwatahadharisha viongozi hao wa shirikisho wakiongozwa na Rais Jamal Malinzi kuwa wasipokuwa makini suala hilo litawafikisha pabaya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox