Shujaa wa MO Bejaia alikuwa ni beki Yassine Salhi aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 20, akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Ismail Belkacemi.

Matokeo hayo yanaifanya MO Bejaia ishike nafasi ya pili katika kundi hilo, nyuma ya TP Mazembe ambayo iliifunga Medeama ya Ghana 3-1 katika mchezo wa kwanza mjiji Lubumbashi Jumapili, wakati Yanga inashika nafasi ya tatu.
Mechi zijazo za kundi hilo, Yanga watakuwa wenyeji wa Mazembe Dar es Salaam na Medeama wataikaribisha Mo Bejaia.
Kikosi kamili cha Yanga kinachoanza ni; Deogratius Munishi 'Dida', Mbuyu Twite, Oscar Joshua/Mwinyi Hajji dk33, Kelvin Yondani, Vicent Bossou, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe/Matheo Anthony dk85 na Deus Kaseke/Geoffrey Mwashiuya dk75.
MO Bejaia; C. Rahmani, A. Messaoudi, A. Lakhdari, S. Baouali, S. Khadir, Y. Salhi/ M. Betorangal dk71, S. Benali, S. Sidibé, M. Ferhat/A. Mouhli dk87, M. Athmani na I. Belkacemi/ B. Bendjelloul dk79.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni