STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 17 Agosti 2016

HESHIMA,REKODI VYOTE VINAFUTWA LEO YANGA VS AZAM.......



KUELEKEA mchezo wa leo Jumatano wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga dhidi ya Azam, kuna mambo mawili lazima yatokee ambayo kwa kila upande yatakuwa na maana kubwa sana.

Mchezo huo ambao ni wa nne mfululizo kwa timu hizo kupambana katika Ngao ya Jamii, utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Ikumbukwe kuwa, mchezo wa Ngao ya Jamii huwakutanisha mabingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la FA, lakini kutokana na Yanga kufanikiwa kuchukua makombe yote hayo, sheria za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zinaelekeza mshindi wa pili wa Kombe la FA ndiye atakayecheza na bingwa wa ligi, ndiyo maana Azam wakapata nafasi hiyo.

Lakini hata kama mshindi wa pili wa ligi ndiye angecheza na bingwa wa ligi, basi Azam ingekuwa tena na nafasi hiyo kwani msimu uliopita imemaliza ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Yanga.

Katika rekodi za Ngao ya Jamii, Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi mara tano katika michezo saba iliyocheza. Mwaka 2001, iliifunga Simba mabao 2-1, mwaka 2009 ikafunga bao 1-0 dhidi ya Mtibwa.

 

Mwaka 2010, Yanga iliifunga Simba kwa penalti 3-1, baada ya mchezo kumalizika kwa suluhu katika muda wa kawaida, lakini mwaka uliofuatia ikafungwa na Simba 2-0.

Baada ya hapo, ikacheza tena mwaka 2013 dhidi ya Azam na kuibuka na ushindi wa bao 1-0, mwaka uliofuatia ikaifunga tena Azam mabao 3-0, kabla ya mwaka jana kushinda kwa penalti 8-7 kutokana na muda wa kawaida kumalizika kwa suluhu.

 

Mara ya kwanza kwa Yanga na Azam kukutana kwenye Ngao ya Jamii ilikuwa ni mwaka 2013 katika mchezo huo wa ufunguzi wa msimu wa 2013/14.

Kuanzia hapo mpaka tunaelekea kuushuhudia mchezo wa leo, Azam haijawahi kuifunga Yanga kwenye mechi tatu mfululizo za Ngao ya Jamii mfululizo timu hizo zilipokutana.

Kutokana na hilo, leo Azam watataka kuiondoa rekodi hiyo mbaya kwao huku Yanga wakitaka kuendeleza ubabe wao kwa Azam kwa lengo la kulinda heshima yao.

 

Rekodi ya Azam katika Ngao ya Jamii

Mara ya kwanza kwa Azam katika historia yake kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii tangu ilipopata nafasi ya kushiriki Ligi Kuu Bara mwaka 2007, ilikuwa ni dhidi ya Simba, hiyo ilikuwa ni mwaka 2012 ambapo ilikubali kichapo cha mabao 3-2.

Miaka mingine mbele baada ya kucheza na Simba, ikapambana na Yanga na mara zote ikapoteza, hivyo mchezo wa leo kwa timu hiyo utakuwa na maana kubwa endapo itaibuka na ushindi.

Matarajio ya wengi katika mchezo huu

Baada ya Azam kulifanyia marekebisho makubwa benchi lake la ufundi kwa kumuondoa Muingereza, Stewart Hall aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho, ikamleta Mhispania, Zeben Hernandez ambaye amekuja na wasaidizi wake kutoka nchini kwao.

Mpaka sasa, kocha huyo amekiongoza kikosi cha Azam kucheza mechi nane za kirafiki, imeshinda sita, sare mbili huku kikiwa hakijapoteza hata mchezo huo.

Kwa maana hiyo, tunaweza kusema Yanga itakumbana na ushindani wa hali ya juu kwani licha ya kocha huyo kuwa na kikosi hicho kwa muda mfupi, lakini tayari ameanza kuonyesha makali yake.

Kwa upande wa Yanga ambayo yenyewe haijapumzika tangu ilipomalizika ligi Mei, mwaka huu kutokana na kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, tunaweza kusema mechi hizo ilikuwa ikizitumia kujiweka fiti zaidi, hivyo wapo vizuri.

Usajili iliyoufanya kwa kuwaongeza nyota kadhaa kikosini kwao, inakifanya kikosi hicho kuwa kipana zaidi, kilichofanywa ni kusubiri mwisho wa mchezo matokeo yatakuaje.

 mdosejr@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox