STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 15 Agosti 2016

MANJI KUIBWAGA YANGA, WANACHAMA WA HAHA, BILIONEA MWINGINE ATAJWA KUOKOA JAHAZI

Habari zilizoenea kwenye mitao ya kijamii ni kwamba Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji ameamua kujiuzulu wadhifa wa uenyekiti katika klabu hiyo pamoja na kusitisha zoezi la kutaka kuikodi timu hiyo kwa miaka 10 kama ilivyokuwa dhamira yake hapo awali.
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya Yanga, inadaiwa kuwa bosi huyo ameamua kukaa pembeni ikiwa ni baada ya kuibu kwa mijadala mikubwa na baadhid ya watu kupinga uamuzi wake wa kutaka kuikodi Yanga.
“Natukanwa sana na baadhi ya matajiri ambao ni wapenzi wa Yanga…hawapendi mimi niwepo pale. Pesa ni yangu natoa kwa mapenzi niliyonayo kwa klabu yangu…kwanini nitukanwe wakati sipati maslahi yoyote? Najiuzulu,” Ni kauli ya mwenyekiti wa Yanga SC ambaye ametangaza kujiuzulu kufuatia kusakamwa na hasa baada ya kuomba kuichukua Yanga kwa miaka 10. (kwa mujibu wa facebook page ya Naipenda Yanga).
Hata hivyo kumekuwa na vikao mbalimbali kumsihi Manji abadili maamuzi yake lakini inaonekana amechoka na ameamua kuibwaga Yanga.
Tayari Reginald Mengi ameonesha nia ya kuingia Yanga endapo Manji ataondoka. Leo jioni baraza la wazee linataraji kuwa na kikao na Mengi.
Chanzo : Shafiih 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox