STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 14 Agosti 2016

MEDEAMA YAITUPA YANGA NJE YA MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO


1
Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Yanga SC, wametupwa nje kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, baada ya TP Mazembe kuchapwa mabao 3-2 na Medeama ya Ghana katika mchezo wa kundi A uliofanyika kunako dimba la Essipong huko Sports Takoradi, Ghana.
Medeama walipata mabao yao kupitia kwa Enock Atta Agyei, Moses Amponsah Sarpong na Kwesi Donsu huku Mazembe wakipata mabao yao yote mawili kupitia kwa Jonathan Bolingi.

Kufuatia matokeo hayo, Medeama ambao mchezo wa mwisho watacheza na MO Bejaia ya watahitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu hatua ya nusu fainali, wakati huo Yanga watakuwa ugenini wakikipa na TP Mazembe mjini Lubumbashi, mchezo ambao utakuwa ni wa kukamilisha ratiba tu kwa upande wa Yanga.

Mpaka sasa, TP Mazembe bado wako kileleni na pointi zao 10 baada ya michezo mitano, wakishinda mara tatu, sare mara moja na kufungwa mara moja, wakifuatiwa kwa karibu na Medeama wenye alama nane, Bejaia wakishika nafasi ya tatu na pointi zao tano na Yanga wakiburuza mkia na pointi zao nne.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox