MSHAMBULIAJI wa Chelsea,
Diego Costa amedai kuwa anafahamu yeye sio malaika pindi awapo uwanjani
na hatabadilika aina yake ya uchezaji wa kutumia nguvu.
Costa amefungwa
mara mbili kutocheza mechi tatu baada ya kumkanyaga mchezaji wa
Liverpool Emre Can na baadae kumpiga kibao beki wa Arsenal Laurent
Koscielny.
Akihojiwa nyota huyo wa kimataifa wa Hispania aliyezaliwa
Brazil mwenye umri wa miaka 27, amesema amefikia hapo alipo kutokana na
jinsi anavyocheza hivyo hawezi kubadilika kwasababu watu wanataka
hivyo.
Costa alihamia Stamford Bridge Julai mwaka 2014 akitokea Atletico
Madrid na kuisaidia Chelsea kushinda taji la Ligi Kuu na Kombe la Ligi
msimu uliopita.
Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini amemtaka
Costa kupunguza mchezo wake wa kutumia nguvu sana, wakati meneja wa
Arsenal Arsene Wenger akimtuhumu mshambuliaji huyo siku kujihusisha na
vurugu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni