Timu ya Manchester United imepata
kipato kikubwa kuliko timu yoyote katika msimu uliopita kulingana na
taarifa zilizochapishwa na kampuni kubwa ya ukaguzi duniani (Deloitte).
Manchester
United imewashinda Real Madrid waliofanya vizuri katika michezo kwa
miaka 11baaada ya kukusanya kipato kikubwa takribani Euro 689 katika
msimu wa 2015-2016.
Clubu za ligi ya Premier imeshuhudia kukua kwa kipato kwa Euro Millioni mia moja
Ukijumlisha
vipato vya timu ishirini bora kwa msimu wa 2015-2016 vimeongezeka kwa
asilimia 12% na kufikia euro billioni 7.4 hii haijawahi kutokea.
Hii ni mara ya kwanza kwa Man U kushikilia nafasi hiyo tokea msimu wa 2003-04.
Real Madrid wameshuka mpaka nafasi ya tatu wakiwaacha wapinzani wao wakubwa Barcelona katika nafasi ya pili. Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wapo nafasi ya
nne huku matajiri wa jiji la Manchester Man City wakiwa nafasi ya tano
kwa kutengeneza Euro milioni524 kwa msimu uliopita.
Hii ni mara ya kwanza kwa city kuingia katika nafasi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni