MKUU
wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Jerry Muro ameomba
msamaha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa adhabu ya kufungiwa mwaka
mmoja kujihusisha na masuala ya soka.
Julai
mwaka jana, Muro alifungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka
pamoja na kutozwa faini ya Sh. Milioni 3 baada ya kukutwa na hatia
katika mashitaka mawili kati ya matatu yaliyowasilishwa na TFF dhidi
yake.
Katika
barua yake kwa TFF, Muro amesema kwamba anakiri kupata barua ya
kufungiwa kutoka Kamati ya Maadili, lakini anaomba msamaha baada ya
kutumikia nusu ya adhabu yake.
Jerry Muro ameomba msamaha TFF kwa adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka
Muro
ameomba apunguziwe adhabu na kurudi kutekeleza majukumu yake kwa
mwajirin wake, Yanga SC kuanzia kipindi hiki cha michuano ya Kombe la
Mapinduzi, inayoendelea visiwani Zanzibar.
Mapema
wiki iliyopita, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa mahasimu,
Simba SC, Hajji Manara alimuombea msamaha Muro pia. Na Wasemaji wa timu
nyingine akiwemo Massau Bwire wa Ruvu Shooting walkimuombea msamaha pia
mwenzao huyo, wakiamini atakuwa amejirekebisha.
Muro
alifungiwa Jukai 8 mwaka jana baada ya kikao cha Kamati ya Maadili ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wake, Wakili
Wilson Ogunde kilichofanyika mjini Dar es Salaam.
Makosa
yaliyomtia hatiani Muro ni kudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF
mwaka 2015 alipotakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5 baada ya kufanya
makosa, lakini amekaidi kulipa hadi leo.
Kwa
kosa hilo akahukumiwa kutengana na masuala ya soka kwa mwaka mmoja-
wakati shitaka lingine lililomtia hatiani ni kuchochea vurugu na
kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho kati ya
Yanga na TP Mazembe ya DRC.
Katika
shitaka hilo, Jerry anadaiwa kuwashawishi mashabiki wa Yanga kuwafanyia
vurugu mashabiki wa Simba kwenye mchezo huo ambao timu yake ilifungwa
1-0 na Mazembe Juni 28, mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa
kosa hilo Jerry Muro alifungiwa mwaka mmoja pia na kutozwa faini ya Sh.
Milioni 3 ingawa adhabu zote zinakwenda sambamba – maana yake atakuwa
pembeni na masuala ya soka kwa mwaka mmoja tu.
Hata
hivyo, Jerry Muro alifanikiwa kuishinda TFF katika shitaka la kupingana
na maamuzi ya shirikisho hilo juu ya masuala ya utoaji wa haki za
matangazo ya Televisheni.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Alhamisi, 5 Januari 2017
JERRY MURO AOMBA MSAMAHA TFF, SOMA BARUA ALIYOIANDIKA HAPA
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni