Mabingwa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, mchana huu imemtangaza, Aristica Cioaba, kuwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho.
Cioaba,
45, raia wa Romania anakuja Azam FC kurithi mikoba ya Mhispania Zeben
Hernandez, aliyesitishiwa mkataba pamoja na benchi lake zima la ufundi.
Kocha
huyo atasaidiana na makocha wazawa, Idd Nassor Cheche na Kocha wa
Makipa Idd Abubakar.
Akizungumza
na mtandao rasmi wa klabu Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Saad
Kawemba, tayari wamefanikiwa kumpata kocha huyo na wameingia naye
mkataba wa muda wa miezi sita wenye kipengele cha kuongezwa.
Alisema
Cioaba ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika na ataiongoza Azam FC kwa
kipindi hiki hadi mwishoni mwa mwa msimu, ambapo baada ya kuisha watakaa
tena mezani kufanya tathimini ya mafanikio yake na wapi wanaweza
kuendelea kutokana na kazi iliyofanyika.
“Bodi
ya Wakurugenzi ya Azam FC inapenda wadau wote wa mpira na wapenzi na
mashabiki wa Azam kwamba klabu imempata mwalimu, ambaye ndiye ataiongoza
klabu kwa kipindi hiki hadi mwishoni mwa msimu.
“Kwa
hiyo kwa mashabiki wetu maana yake ni kwamba tukiingia kwenye mechi
inayofuata ya ligi, kocha atakuwa ameanza kazi na Cheche (Idd Nassor)
atakuwa msaidizi wake na benchi lake zima alilokuwa nalo hivi sasa
litaendelea,” alisema.
Kawemba
aliongeza kuwa hivi sasa kocha huyo atakuwa na kikosi visiwani Zanzibar
kufuatilia mwenendo wa timu ulivyo na ataendelea kutoa ushauri
panapohitajika na ataanza rasmi kukaa kwenye benchi mpaka pale vibali
vyake vya kufanya kazi nchini vitakapokamilika.
“Taratibu
hizo zitakwenda kwa mujibu wa sheria za nchi, ambapo tutaziheshimu na
kuona ya kwamba tutazifanya kwa haraka zaidi ili mwalimu aweze kupata
kibali cha kufanya kazi hapa nchini, kwa hayo machache tunawaomba
mashabiki wetu wawe watulivu wampe sapoti kocha na wadau wote wa mpira
waone ya kwamba tumefanya jambo la kheri,” alisema.
WAKATI HUO;
BAO pekee la kiungo Frank Raymond Domayo limetosja kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Taifa Jang’ombe katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Domayo alifunga bao hilo dakika ya 33 kwa shuti la umbali wa mita 19, baada ya kuwazidi mbinu viungo wa Taifa Jang’ombe.
Na kwa ushindi huo, Azam FC inakwenda fainali ambako itakutana na mshindi kati ya Simba na Yanga Ijumaa. Simba na Yanga zitamenyana kuanzia Saa 2:15 usiku wa leo katika Nusu Fainali ya pili Uwanja wa Amaan.
Pamoja na kufungwa, Taifa Jang’ombe walicheza vizuri na kutengeneza nafasi, lakini bahati haikuwa yao jioni ya leo.
Kikosi
cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe/Himid Mao dk46,
Gardiel Michael, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Stephan Mpondo/Abdallah
Kheri dk79, Joseph Mahundi/Enock Atta Agyei dk75, Frank Domayo, Salum
Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’ na Yahya Mohammed/Shaaban
Iddi dk59.
Taifa
Jang’ombe; Ahmed Suleiman, Omary Yussuf, Hassan Msabah, Abdallah
Shaibu, Samir Yahya, Khatib Simai/Arafat Suleiman dk53, Adam Ibrahim,
Ali Mkanga, Yahya Tumbo/ally badru dk53, Meta Apingi/Hassan Salum dk74
na Mohammed Said.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni